Uboreshaji
wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia mfumo wa Biometric
Voters Registration (BVR) ulikamilika tarehe 04/08/2015 katika Mikoa
yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
Baada
ya kukamilika kwa zoezi la Uboreshaji Tume imekuwa ikichakata
(processing) taarifa za Wapiga Kura ili kuweza kuandaa Daftari la Awali
la Wapiga Kura, katika maandalizi hayo mifumo imeweza kugundua kasoro
mbali mbali ambazo baadhi zimefanyiwa kazi na zingine zinaendelea
kufanyiwa kazi, kasoro hizo ni pamoja na Wapiga Kura Kujiandikisha zaidi
ya mara moja.
Mfumo
wa BVR unao mfumo mdogo wa “Mini AFIS” unaoweza kubaini Mpiga Kura
anayataka kujiandikisha zaidi ya mara moja katika kituo husika, mfumo
huo ulikuwa umeandaliwa ili kuweza kubaini Wapiga Kura wanaotaka
kujiandikisha zaidi ya mara moja na kuzuia Uandikishaji huo katika BVR
Kit yoyote. Hii ingewekana iwapo Mfumo wa mawasiliano ungekuwa na nguvu
katika vituo vyote na kuweza kuwasiliana na mifumo iliyoko katika kituo
kikuu cha maandalizi ya Daftari(Data Processing Center) kwani katika
kituo hicho imewekwa mifumo ya hali ya juu inayoongoza kimataifa katika
kulinganisha alama za vidole na kubaini waliojiandikisha zaidi ya mara
moja.
Kwa
kutokuwa na mawasiliano yenye nguvu kutoka katika kila kituo Tume
ilianza kulinganisha taarifa za Wapiga Kura mara tu baada ya taarifa
kufikishwa katika kituo cha maandalizi ya Daftari hivyo kwa mitambo
iliyopo Tume imebaini Wapiga Kura wote waliojiandikisha Zaidi ya mara
moja ambao taarifa zao zimeisha chakatwa ambao kwa sasa imefikia 52,062
Idadi hii inaweza kuongezeka au kupungua kulingana na uchakataji wa
taarifa.
Baadhi ya vituo kutokuwa na Wapiga kura.
Tatizo
hili linasababishwa na maombi ya kuanzishwa kwa vituo wakati zoezi la
Uandikishaji limeanza, baadhi ya vituo hivyo havikutumika wakati wa
Uandikishaji kama ilivyokusudiwa kwa sasa Tume inafanyika kazi ya
kuhamisha Wapiga Kura na kuwapeleka katika vituo hivyo ili kuwapunguzia
umbali mrefu kutoka kwenye vituo walivyojiandikisha wakati wa zoezi la
Uandikishaji, kazi hii Tume inaendelea kuifanya kwa kushirikiana na
watendaji wa Kata katika Halmashauri husika.
Baadhi ya Vituo kuwa na Wapiga Kura wachache au Wengi katika Vituo vya Uandikishaji.
Tatizo
hili pia lilisababishwa na vituo kuongezwa wakati zoezi la Uandikishaji
limeanza. Kabla ya kuongezwa vituo katika BVR kutokana na hamasa ya
Wapiga Kura Kujiandikisha Wapiga Kura hao walianza kujiandikisha katika
vituo vingine na baada ya kuongeza vituo katika BVR vituo vilivyoongezwa
viliendelea kufanya Uandikishaji kwa siku mbili au tatu za mwisho hivyo
kuonekana kama vina Wapiga Kura wachache, kasoro hiyo inarekebishwa pia
kwa kusaidiana na watendaji wa Kata husika ili kuwahamisha Wapiga Kura
waliojiandikisha katika vituo kabla ya kuongeza kwenye BVR vituo
vilivyoombwa kuongezwa na kupelekwa kwenye vituo karibu na maeneo
wanayoishi.
Wapiga kura kuandikishiwa katika Mfumo wa Mafunzo.
Katika
taarifa zilizochakatwa imebainika kuwa baadhi ya Wapiga Kura
waliandikishwa kwa kutumia mfumo wa mafunzo uliowekwa katika katika BVR
kit iliyotakiwa kutumika wakati wa mafunzo tu, Usahihi wa taarifa za
Biometric za Wapiga Kura hao kuwa sahihi lakini baadhi ya taarifa
nyingine kuhitaji marekebisho kutoka katika fomu za Uandikishaji
zilikizojazwa. Kazi hiyo inaendelea kufanyika katika kitu cha maandalizi
ya Daftari kwa kuwa fomu zote za uandikishaji zimeishafika. Marekebisho
hayo yalichelewesha kidogo baadhi ya taarifa katika madaftari
yaliyowekwa wazi. Kazi ya Kurekebisha kasoro hizo zimeendelea
kurekebishjwa na kabla ya tarehe 05/09/2015 kasoro zote zitakuwa
zimerekebishwa.
Baadhi ya Taarifa za Wapiga Kura kutochukuliwa taarifa zao katika BVR Kit.
Tatizo
hili lilisababisha baadhi Wapiga kura kutoonekana katika vituo
walivyojiandikisha, zipo baadhi ya BVR Kit ziliibiwa na zikafanyika
jitihada za kung’oa baadhi ya vifaa katika BVR kama vile Laptop na vifaa
vingine. Zipo BVR mbili (2) kati ya BVR Kit 8000 ziliibiwa na walioiba
walifanya jitihada za kuiba baadhi ya vifaa katika BVR kit hizo, BVR Kit
hizo zilipatikana lakini zikiwa katika hali mbaya ya Uaribifu hivyo
kushidwa kuondoa taarifa za Wapiga Kura mara moja, kwa kuwa Tume iliweka
vifaa mahususi inapojitokeza changamoto kama hiyo kutopoteza taarifa za
Wapiga Kura, chombo hicho kinachohifadhi taarifa za Wapiga Kura mara
inapotokea uaribifu mbukbwa hususan wa kompyuta kuweza kupata taarifa za
Wapiga Kura bila tatizo, Tume tayari imekwisha pata vifaa vilivyokuwa
vimeifadhi taarifa za Wapiga kura na tayari taarifa hizo zinaingizwa
katika mfumo wa kuchakata taarifa za Wapiga Kura.
Kata Mpya.
Kwa
mujibu wa sheria OWM TAMISEMI ndiyo yenye hadhi ya kupandisha na
kugawa maeneo ya kiutawala ili kuchochea maendeleo ya haraka kwa
wananchi wake. Mabadiliko hayo ya mipaka ya kiutawala yanahitaji
kuhuishwa na Tume katika Mifumo yake ili kuwezesha chaguzi kufanyika na
hasa chaguzi za madiwani, hivyo yanafanyika marekebisho ya kuhamisha
kuweka vituo na Wapiga Kura katika maeneo mapya ya kiutawala
yaliyoanzishwa, ikiwa ni pamoja na: Vitongoji, Mitaa,Vijiji, Kata na
Halmashauri.
Baadhi ya Taarifa za Wapiga Kura taarifa zao kukosewa na BVR Kit Opereta wakati wa Uandikishaji.
Baadhi
ya Wapiga kura taarifa zao zilikosewa na BVR Opereta wakati wa
Uandikishaji hivyo kuhitaji marekesho na kupatiwa kadi mpya. Tume
ilipeleka BVR Kit katika Halmashauri zote wakati wa kuweka wazi Daftari
la Awali la Wapiga Kura, ili kufanya marekebisho ya taarifa za Wapiga
kura pale panapohitajika. Marekebisho yamefanyika Tume inategemea
Taarifa hizo zitafika na kuingizwa katika mifumo ili kupata taarifa
sahihi.
Wapiga Kura Kujiandikishia katika maeneo tofauti na maneo wanayoishi.
Baadhi
ya Wapiga Kura walijiandikisha katika maeneo tafauti na maeneo
wanyaoishi, hivyo kuhitaji kuhamisha taarifa zao, tatizo hili
limebainika katika maeneo mengi ya mjini, hasa kwa Wapiga Kura kutaka
kuwahi kupata kadi za Mpiga kura, kasoro hii imeendelea kurekebishwa
wakati wa zoezi la kuweka wazi Daftari.
Uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura.
Uwekaji
wazi wa Daftari la awali la Wapiga Kura ni takwa la kisheria, kifungu
cha 11a cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 kinaitaka Tume
kuweka wazi Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uhakiki wa Taarifa na
kurekebisha kasoro zozote zinalizojitokeza.
Ili
kuhakiki taarifa katika Daftari la Awali la Wapiga Kura wananchi
wanatakiwa kufika katika Ofisi za kata ili kuweza kuangalia kama majina
yao yapo katika Daftari, na ikiwa Taarifa zao ni sahihi mfano Jina,
Jinsia, Tarehe ya kuzaliwa na Kituo chake cha kujiandikishia, Aidha, kwa
Wapiga kura waliohama kata au jimbo moja kwenda kata au jimbo lingine
wanatakiwa kuhamisha taarifa zao.
Zoezi
hili la uhakiki lilianza rasmi tarehe 07/08/2015 katika Mikoa mbali
mbali na limekuwa likiendelea hadi sasa ili kuhakikisha kila Mpiga kura
aliyeandikishwa kupiga kura anaweza kupiga kura bila usumbufu wowote.
Katika
zoezi hili Tume imeweka utaratibu wa kuwaondoa watu wote
waliojiandikisha katika Daftari ambao siyo raia wa Tanzania, ambapo
mchakato huo unaishia katika mahakama ya wilaya. Ili kasoro hii iweze
kuondolewa Tume inahitaji kwa kiasi kikubwa Ushirikiano na wananchi
wanaoishi nao ili kuwawekea pingamizi na waweze kuondolewa katika
Daftari, ni ukweli kwamba iwapo wananchi watawaficha na kutowawekea
pingamizi tatizo hili litakuwa gumu kwa Tume kulitatua.
Kasoro
mbalimbali zilizobainika wakati wa Uandikishaji Tume itahakikisha
inazirekebisha ili kuhakikisha kuwa Tume inakuwa na Daftari sahihi na la
kuhaminika.
Imetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
0 comments :
Post a Comment