Bi. Samia Hassan Suluhu akipokewa na baadhi ya viongozi na makada wakiwa kwenye mkutano huo. Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.[/caption]
BAADHI
ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamelazimika
kuuzuia msafara wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais leo alipokuwa
njiani akitokea Wilaya ya Same kuelekea Wilayani Mwanga mkoani
Kilimanjaro huku wakimuomba awasalimu na kuzungumza nao, kabla ya
kuendelea na safari yake.
Bi.
Samia Suluhu alilazimika kuusimamisha msafara wake baada ya wananchi hao
kusogea zaidi barabarani wakati akipita huku wakinyoosha mikono ya
kumuomba asimame ili azungumze nao eneo la kilometa chache kabla ya
kuingia njia panda.
Wananchi
hao wengi wakiwa wakinamama walimsimamisha kwa kuingia pembezoni mwa
barabara alipokuwa akipita na hivyo kulazimika kusimama kwa dakika
chache na kuzungumza nao.
Akizungumza aliwaambia amefarijika na kuwaona na mapenzi makubwa na
chama chao hivyo kuwaeleza kuwa yeye ni mwanamke pia na anajua kwa
karibu kero ambazo wanakabiliana nazo akinamama sehemu mbalimbali na
kuahidi endapo watapata ridhaa pamoja na Dk. John Magufuli atahakikisha
anasimamia vizuri utaratibu wa kuwawezesha akinamama kupitia vikundi vya
kijamii ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na familia zao.
Alisema
yeye ni mwanamke mzazi anatambua shida wanazokumbana nazo akinamama
hasa kwenye wodi za wazazi hivyo akifanikiwa kuingia madarakani
atahakikisha anasimamia ipasavyo ilani ya chama ambayo imeeleza vizuri
juu ya uboreshaji huduma za afya ikiwemo wodi za akinamama na hali ya
upatikanaji madawa.
"...Matatizo
ya wanawake nayafahamu vizuri wala sisimuliwi maana na mimi ni mzazi
nimeingia wodi ya wazazi mkitupa ridhaa na mwenzangu (mgombea urais, Dk.
Magufuli) nitahakikisha nayasimamia haya vizuri," alisema Bi. Suluhu
akizungumza muda mfupi na wananchi waliomzuia barabarani wakiomba
awasalimu.
Alisema
kero ya maji imekuwa inawatesa akinamama kwa kutumia muda mwingi
kutafuta maji na kushindwa kuzalisha uchumi wa familia ipasavyo, hivyo
Serikali ya CCM imeanza mradi wa kutoa maji katika Bwawa la Nyumba ya
Mungu na kuyaingiza katika vijiji vyenye shida ya maji.
Aidha
akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara Mwanga ameisikia kero ya
uhaba wa mabweni kwa wanafunzi wa kike suala ambalo linachangia kwa
kiasi kikubwa mabinti hao kutiwa mimba na kukatisha masomo eneo hilo na
kudai suala hilo lipo katika ilani ya CCM mwaka huu na litashughulikiwa
vizuri endapo watapewa ridhaa na wananchi, ikiwa ni pamoja na suala zima
la kupambana na kuongeza fursa za vijana ili kukabiliana na uhaba wa
ajira.
Alisema Serikali iliyopita imejitahidi kuongeza huduma za umeme katika
vijiji ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi lakini katika awamu hii CCM
ikipewa ridhaa itahakikisha vijiji vilivyobaki kwa baadhi ya maeneo
vinawekewa umeme.
Alisema
anawapa akinamama kazi kuhakikisha Dk. Magufuli na wagombea wa CCM eneo
hilo wanashinda kwa asilimia 80 kwani wao ndio wenye ushawishi mkubwa
katika familia. Vivyo hivyo kuwataka madiwani wanaogombea kuhakikisha
mgombea uraisi na wengine wanapata kura za kutosha ili kushinda
uchaguzi.
Kwa upande wake Asumta Mshana aliyekuwa mbunge wa CCM na uchaguzi huu
aligombea na kura hazikutosha alisema anawashangaa wanachama ambao
waligombea ndani ya Chama Cha Mapinduzi na waliposhindwa wakaamua
kuondoka ndani ya chama hicho.
Alihoji
kwani walipokuwa wakiomba nafasi hizo hawakutambua kuna kushindwa na
kushinda? Aliwafananisha wanaofanya hivyo ni sawa na akinababa wanaoamua
kukimbia familia zao jambo ambalo ni aibu.
"Nawashauri wababi ndani ya chama na kukijenga chama ili kiweze kufanya
vizuri, kama kura hazikutosha safari hii usikimbie chama kwani mlikuwa
hamjui kuna kushinda na kushindwa unapoomba uongozi," alisema.
Naye Mwenyekiti wa CCM, Mkoa Idd Juma Mohamed alimshukuru Bi. Samia kwa
kuamua kuanza kampeni katika mkoa wake na kumuhakikishia watahimiza
wapiga kura kwani Kilimanjaro bado ni ngome ya CCm na watahakikisha
wanatwaa majimbo yote, viti vya udiwani.
Kawaida;
Wananchi Wamzuia Mgombea Mwenza wa CCM Barabarani Mwanga
BAADHI ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamelazimika
kuuzuia msafara wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais leo alipokuwa
njiani akitokea Wilaya ya Same kuelekea Wilayani Mwanga mkoani
Kilimanjaro huku wakimuomba awasalimu na kuzungumza nao, kabla ya
kuendelea na safari yake.
Bi. Samia Suluhu alilazimika kuusimamisha msafara wake baada ya wananchi
hao kusogea zaidi barabarani wakati akipita huku wakinyoosha mikono ya
kumuomba asimame ili azungumze nao eneo la kilometa chache kabla ya
kuingia njia panda. Wananchi hao wengi wakiwa wakinamama walimsimamisha
kwa kuingia pembezoni mwa barabara alipokuwa akipita na hivyo kulazimika
kusimama kwa dakika chache na kuzungumza nao.
Akizungumza aliwaambia amefarijika na kuwaona na mapenzi makubwa na
chama chao hivyo kuwaeleza kuwa yeye ni mwanamke pia na anajua kwa
karibu kero ambazo wanakabiliana nazo akinamama sehemu mbalimbali na
kuahidi endapo watapata ridhaa pamoja na Dk. John Magufuli atahakikisha
anasimamia vizuri utaratibu wa kuwawezesha akinamama kupitia vikundi vya
kijamii ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na familia zao.
Alisema yeye ni mwanamke mzazi anatambua shida wanazokumbana nazo
akinamama hasa kwenye wodi za wazazi hivyo akifanikiwa kuingia
madarakani atahakikisha anasimamia ipasavyo ilani ya chama ambayo
imeeleza vizuri juu ya uboreshaji huduma za afya ikiwemo wodi za
akinamama na hali ya upatikanaji madawa.
"...Matatizo ya wanawake nayafahamu vizuri wala sisimuliwi maana na mimi
ni mzazi nimeingia wodi ya wazazi mkitupa ridhaa na mwenzangu (mgombea
urais, Dk. Magufuli) nitahakikisha nayasimamia haya vizuri," alisema Bi.
Suluhu akizungumza muda mfupi na wananchi waliomzuia barabarani
wakiomba awasalimu.
Alisema kero ya maji imekuwa inawatesa akinamama kwa kutumia muda mwingi
kutafuta maji na kushindwa kuzalisha uchumi wa familia ipasavyo, hivyo
Serikali ya CCM imeanza mradi wa kutoa maji katika Bwawa la Nyumba ya
Mungu na kuyaingiza katika vijiji vyenye shida ya maji.
Aidha akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara Mwanga ameisikia kero
ya uhaba wa mabweni kwa wanafunzi wa kike suala ambalo linachangia kwa
kiasi kikubwa mabinti hao kutiwa mimba na kukatisha masomo eneo hilo na
kudai suala hilo lipo katika ilani ya CCM mwaka huu na litashughulikiwa
vizuri endapo watapewa ridhaa na wananchi, ikiwa ni pamoja na suala zima
la kupambana na kuongeza fursa za vijana ili kukabiliana na uhaba wa
ajira.
Alisema Serikali iliyopita imejitahidi kuongeza huduma za umeme katika
vijiji ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi lakini katika awamu hii CCM
ikipewa ridhaa itahakikisha vijiji vilivyobaki kwa baadhi ya maeneo
vinawekewa umeme. Alisema anawapa akinamama kazi kuhakikisha Dk.
Magufuli na wagombea wa CCM eneo hilo wanashinda kwa asilimia 80 kwani
wao ndio wenye ushawishi mkubwa katika familia. Vivyo hivyo kuwataka
madiwani wanaogombea kuhakikisha mgombea uraisi na wengine wanapata kura
za kutosha ili kushinda uchaguzi.
Kwa upande wake Asumta Mshana aliyekuwa mbunge wa CCM na uchaguzi huu
aligombea na kura hazikutosha alisema anawashangaa wanachama ambao
waligombea ndani ya Chama Cha Mapinduzi na waliposhindwa wakaamua
kuondoka ndani ya chama hicho.
Alihoji
kwani walipokuwa wakiomba nafasi hizo hawakutambua kuna kushindwa na
kushinda? Aliwafananisha wanaofanya hivyo ni sawa na akinababa wanaoamua
kukimbia familia zao jambo ambalo ni aibu.
"Nawashauri wababi ndani ya chama na kukijenga chama ili kiweze kufanya
vizuri, kama kura hazikutosha safari hii usikimbie chama kwani mlikuwa
hamjui kuna kushinda na kushindwa unapoomba uongozi," alisema.
Naye
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa Idd Juma Mohamed alimshukuru Bi. Samia kwa
kuamua kuanza kampeni katika mkoa wake na kumuhakikishia watahimiza
wapiga kura kwani Kilimanjaro bado ni ngome ya CCm na watahakikisha
wanatwaa majimbo yote, viti vya udiwani.
0 comments :
Post a Comment