……………………..
Viongozi
wa dini hapa nchini wametakiwa kutoruhusu wanasiasa kuyatumia madhabahu
yao na nyumba za ibada kuzungumzia mambo ya kisiasa katika wakati huu
wa uchaguzi ili kuilinda amani hapa nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la wakristo hapa nchini na
Askofu wa kanisa la Aglikana la mt.Kilimanjaro Stanley Hotay kwenye
kongamano la mbegu ya amani Tanzania lililofanyika jijini hapa na
kuwashirikisha viongozi wa madhehebu ya kikristo kanda ya kaskazini.
Alisema
kuwa mimbari zetu zisitumiwe kinyume cha sheria kwa kuwaelekeza waumini
wao kuhusu mgombea ama chama cha siasa cha kukichagua wao wapewe uhuru
wa kufanya maamuzi yao ni yupi wa kumpa kura zao kwa kuwa wanasiasa hao
wote ni waumini wao.
Aliwataka
viongozi hao wa dini kukataa rushwa za pesa,na bakshishi zingine kwa
ahadi ya kulindwa na kupewa nyadhifa za kuteuliwa iwapo wanasiasa hao
watapata nafasi hilo ni suala la kuliepuka kabisa.
‘’Mikusanyiko
sio kipindupindu tukatae kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa kuwanadi
wagombea na pia kwenye nyumba zetu za ibada kutompigia debe mwanasiasa
yeyote hiyo itatuepusha na kuvuruga haki ya waumini wetu ya kujichagulia
wanaomuona anawafaaa’’alisema Hotay.
Aidha
alilitaka jeshi la polisi hapa nchini kupitia kwa mkuu wa jeshi hilo
Ernest Mangu kuangalia kutenganisha Maandamano,Mikutano ya hadhara na
mikusanyiko mbali mbali ya kidini na kisiasa kwamba vibali vya
mikusanyiko ya kisiasa wapewe wakuu wa polisi na vibali vya mikusanyiko
ya kidini wapewe wakuu wa wilaya.
Alisema
kuwa hilo litaepusha jeshi la polisi au waziri kutoa adhabu ya jumla na
kusababisha viongozi wa dini pamoja na waumini wao kujenga chuki kubwa
kwa serikali yao na kusababisha viongozi wa kidini kufikia kuzungumzia
katika vikao vya mara kwa mara kwamba serikali inaagenda ya siri na
viongozi wa dini.
Alikemea
siasa za matusi na kuchafuana katika majukwaa na badala yake aliwataka
kutumia lugha za staha na kuheshimiana,huku akiwataka kutoa uhuru wao wa
siku ya jumapili kuabudu badala ya kuifanya ndio siku ya uchaguzi.
0 comments :
Post a Comment