Naibu
katibu mtendaji kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Mipango anayesimamia
klasta ya Miundombinu na huduma, mhandisi Happiness Mgalula akitoa
hotuba katika mkutano uliowahusisha ujumbe wa wadau wa maendeleo ya
viwanda kutoka Tanzania na ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini China.
Wajumbe wa mkutano wakiwa wanafuatilia kwa makini mada zinazowasilishwa katika mkutano wa wadau wa maendeleo ya viwanda.
Naibu
katibu mtendaji kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango anayesimamia
klasta ya bishara za kimataifa na mahusiano ya uchumi, Bw. Paul
Sanagawe akihutubia wajumbe wa kikao ambao ni wadau wa maendeleo ya
viwanda kutoka China na Tanzania.
Wajumbe
wa mkutano wakifuatilia mada inayotolewa na Mkurungenzi wa viwanda
kutoka wizara ya viwanda na biashara mhandisi Elli Pallangyo.
Mkurungenzi wa viwanda kutoka wizara ya viwanda na biashara mhandisi Elli Pallangyo akitoa mada kwa wajumbe wa mkutano.
Mkurugenzi
mtendaji wa sekta binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye akisisitiza jambo
wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano ambapo aliisifu serikali kwa
kujitahidi kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa sekta binafsi.
Mkurugenzi
wa kituo cha uwekezaji Tanzania (CTI) Bibi Juliet Kairuki akitoa mada
katika mkutano kati ya wadau wa maendeleo ya viwanda kutoka China na
Tanzania.
Picha ya pamoja kati ya wadau wa maendeleo ya viwanda kutoka Tanzania na ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini China.
Wajumbe
wa mkutano wakisikiliza kwa makini hotuba kutoka kwa Naibu katibu
mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Mhandisi Happiness Mgalula
wakati wa mkutano.
Wajumbe wa mkutano wakiwa wanasoma kwa makini baadhi ya nyaraka katika mkutano huo.
Mkurugenzi
mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (CTI) Bibi Juliet Kairuki
(kulia) akibadilishana mawazo na kaimu mkurugenzi wa NDC bw. Mlingi
Mkucha nje ya ukumbi wa mkutano.
Wajumbe wa mkutano wakiwa wanasikiliza kinachoendelea ndani ya mkutano wa wadau wa maendeleo ya viwanda.
Na Adili Mhina.
Wadau
wa maendeleo ya viwanda nchini wametumia vyema fursa ya kutangaza na
kuwashawishi wawekezaji wa kigeni kutoka nchini China kuwekeza katika
maeneo muhimu yatakayohimiza maendeleo ya viwanda na kupunguza umaskini
miongoni mwa wananchi.
Hayo
yametokea katika mkutano wa siku mbili mfululizo kati ya wadu wa
maendeleo ya viwanda kutoka serikalini, sekta binafsi nchini pamoja na
ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini China uliomalizika jana. Mkutano huo
ulioandaliwa na kituo cha kimataifa cha kupunguza umaskini cha nchini
China, Mfuko wa maendeleo wa China-Afrika kwa kushirikiana na kituo cha
uwekezaji Tanzania na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ulibeba ujumbe
usemao, “punguza umaskini kupitia maendeleo ya viwanda”.
Katika
hotuba yake kwa niaba ya katibu mtendaji wa Ofisi ya Rais Tume ya
mipango, naibu katibu mtendaji anayesimamia klasta ya miundo mbinu na
huduma mhandisi Hapness Mgalula alisema Mkutano huo umekuja wakati
muafaka ambapo Tanzania ipo katika maandalizi ya kuandaa mpango wa
maendeleo wa miaka mitano (2016/17-2020/21) ambao umebeba dhima ya
kuendeleza uchumi wa viwanda. “mkutano huu sio kwamba tu umekuja wakati
muafaka lakini pia ni muhimu kwa sababu miongoni mwa yatakayojadiliwa
hapa yatatumika katika kuboresha huo mpango”, alisema Mgalula.
Kwa
upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC),
bi Juliet Kairuki aliueleza ujumbe kutoka China kuwa kuwa Tanzania kuna
maeneo mbali mbali ya uwekezaji ambayo yanaweza kuleta tija kubwa kwa
Taifa pamoja na wawekezaji.
Alisisitiza
zaidi kwa wawekezaji hao kuwekeza katika kujenga viwanda nchini ili
kuondokana na usafirishaji bidhaa ghafi kwenda nchi za nje. Miongoni mwa
maeneo aliyoyawekea msisitizo katika uwekezaji wa ujenzi wa viwanda ni
pamoja na; ubanguaji wa korosho, usindikaji wa mbegu za mafuta,
utengenezaji wa nguo, ngozi, utengenezaji wa nyama bora na maziwa.
Alisisitiza
kuwa pamoja na kuwa uwekezaji wa ujenzi wa viwanda katika maeneo hayo
utasaidia kukuza ajira kwa wanachi vilevile utasaidia kuongeza thamani
ya bidhaa zinazotoka nchini kwenda kuuzwa nchi za nje. “kwa sasa bidhaa
nyingi zinauzwa zikiwa ghafi na hii inafanya kuuza bidhaa bei ya chini
wakati kama tukifanikiwa kujenga viwanda na kuuza bidhaa za viwandani
thamani ya mazao yetu itaongezeka na italeta faida upande wa serikali na
vilevile kwa muwekezaji,”.
Nae
mkurugenzi wa viwanda kutoka wizara ya viwanda na biashara mhandisi
Elli Palangyo aliwahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu salama
kwa uwekezaji hivyo yeyote anayekuja kuwekeza ajue kuwa yupo katika eneo
salama na lenye tija kibiashara.
Alieleza
kuwa Tanzania ina faida nyingi za kuwavutia wawekezaji ikiwa ni pamoja
na kuwepo kwa amani na utulivu wa taifa toka kipindi cha uhuru, uwepo wa
maliasili za kutosha kama vile madini na gesi asilia, upatikanaji wa
ardhi ya kutosha na yenye rutuba kwa ajili ya kilimo, kuwepo kwa bahari
inayotumika kupitisha bidhaa mbalimbali hususani kwenye nchi zisizo na
bahari, na zingine nyingi.
Kwa
upande wa Zanziabar Mkurugenzi wa uwekezaji kutoka mamlaka ya
uwekezaji vitega uchumi Zanzibar (ZIP) Nasriya Nassor alieleza wadau
kuwa Zanzibar ina fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta za utalii,
uvuvi, kilimo pamoja na maeneo mengine kama huduma za kifedha,
usafirishaji, nishati pamoja na huduma mbalimbali za jamii.
Wawekezaji
hao kutoka nchini China walionesha kuridhishwa na uwepo wa fursa
mbalimbali zilizopo nchini na kueleza kuwa katika kutimiza azma ya
kupunguza umaskini kupitia maendeleo ya viwanda Tanzania, China ina
jukumu kubwa hususani katika kutoa mawazo, uzoefu, elimu, fursa na
kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
0 comments :
Post a Comment