Wasanii
wenye vipaji vya kuimba wakihakiki majina yao kwa DJ Haazu, wa Radio 5
wakati wa mchakato wa RADIO 5 KAMATA KIPAJI uliofanyika katika viwanja
vya TP SINZA Jijini Dar es salaam Septemba 12, 2015.wenye lengo la
kusaka vijana wenye vipaji na kuwainua
kutokana na vipaji vyao.
Katika kuonyesha kuwa wapo karibu
na vijana wa kitanzania katika kuwasaidia kuwainua kiuchumi na
kiuwezo,kituo cha Radio maarufu kutoka kaskazini mwa Tanzania ARUSHA
Radio 5 kimenzisha mchato maalum wa kusaka vipaji kwa vijana wa
kitanzania mchakato ambao umeanzia Jijini Dar es salaam ukiwa na lengo
la kuhakikisha kuwa wanamuwezesha kijana mwenye kipaji kufikia malengo
na ndoto zake
DJ Haazu akiwajibika.
Radio 5 imekuwa na michakato
mbalimbali ili kusaidia vijana katika secta tofauti tofauti zinazohusu
maisha yao ya kiuchumi huku ikiwa inawaunga mkono vijana wenye shughuli
mbalimbali ambao hufika radioni hapo kuomba saport ikiwa ni pamoja na
vijana wa sarakasi,ujasiriamali na fani nyingine.
Mchakato ambao sasa unatajwa kuwa utakuwa msaada mkubwa kwa vijana ambao umezinduliwa Jijini Dar es salaam na kupewa jina la RADIO 5 KAMATA KIPAJI katika viwanja vya TP sinza darajani ilishughudiwa vijana wengi wakijitokeza kuonyesha vipaji vyao ili waweze kuibuka na zawadi mbalimbali ambazo zinatolewa na waandaji hao.
Mchakato ambao sasa unatajwa kuwa utakuwa msaada mkubwa kwa vijana ambao umezinduliwa Jijini Dar es salaam na kupewa jina la RADIO 5 KAMATA KIPAJI katika viwanja vya TP sinza darajani ilishughudiwa vijana wengi wakijitokeza kuonyesha vipaji vyao ili waweze kuibuka na zawadi mbalimbali ambazo zinatolewa na waandaji hao.
WAfanyakazi
wa RADIO 5 wakishangilia wakati Wasanii mbalimbali ambao ni vijana
wenye vipaji wakati wakionesha vipaji vyao jukwaaji (kulia), Mtangazaji
wa Redio 5 Mwangaza Jumanne (katikati), Meneja masoko na mawasiliano
Sarah Keiya na kushoto ni Meneja Vipindi, Mathew Philip.
Katika zoezi hilo vijana
walitakiwa kutuma nyimbo zao radioni ikiwa ni pamoja na kujiandikisha
majina yao ili siku waandaaji hao watakapofika katika mtaa waliopo basi
waweze kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao,na kupatikana washindi
ambapo mchakato huo utapita katika maeneo yote ya jiji la Dar es salaam
na mwisho kuwapata washindi wanne ambao ndio watakaoibuka na zawadi
kabambe.
Lengo kuu la mchakato huo ni kuwasaka vijana ambao wanavipaji na wapo mtaani kutokana na sababu mbalimbali ambazo wameshindwa kuonyesha vipaji hivyo ambapo RADIO 5 wameamua kupita katika mitaa hiyo kuhakikisha kuwa vijana hao wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji walivyo navyo kwa watanzania.
Lengo kuu la mchakato huo ni kuwasaka vijana ambao wanavipaji na wapo mtaani kutokana na sababu mbalimbali ambazo wameshindwa kuonyesha vipaji hivyo ambapo RADIO 5 wameamua kupita katika mitaa hiyo kuhakikisha kuwa vijana hao wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji walivyo navyo kwa watanzania.
Umati wa mashabiki waliojitokeza kushuhudia wasanii wenye vipaji jukaani.
Wakati zoezi hilo likiendelea
mtandao huu ulipata nafasi ya kuzngumza na mkurugenzi wa RADIO 5 Bw
ROBERT FRANCIS ambaye amesema kuwa ni jambo jema kuona kazi hilo imeanza
kwa amani na furaha hivyo watanzania waendelee kuwaunga mkono huku
akiwataka vijana mbalimbali wenye vipaji mkoani Dar es salaam kuendelea
kujitokeza maeneo mbalimbali ambapo ziezi hilo litakuwa linafanyika
pamoja na kuendelea kusikiliza Radio hiyo.
Naye meneja vipindi wa RADIO 5
Ndugu MATHEW PHILIP Akizungumza na mtaandao huu wakati zoezi hilo
likiendelea amesema kuwa kupitia vipindi vya Radio hiyo hasa vipindi vya
kutafuta vipaji nyumba kwa nyumba Dar es salaam vijana wataweza kuinua
vipato vyao huku akisisitiza kuwa watanzania waendelee kusikiliza RADIO 5
kwani kuna mambo mengi na mazuri yanaendelea kuwajia.
Msanii akilimiki jukwaa.
Meneja biashara wa kituo hicho cha
Radio Bi ANGELA MAINA alisema kuwa maana halisi ya kufanya zoezi hilo
ni kuwapa vijana nafasi ili kukuza vipaji vyao hasa katika tasnia ya
music ili miaka ijayo watanzania waone matunda ya kazi hiyo haswa kwa
washiriki wa zoezi hilo.
Aidha meneja masoko na mahusiano
wa RADIO 5 Bi SARAH LAZARO alisema kuwa pamoja na lengo kuu la mchakato
huo ni kuvumbua na kunyanyua vipaji lakini pia ni nafasi kwa wadau wa
biashara na mashirika binafsi haswa yanayojihusisha na maswala ya
kijamii kuanza sasa kushirikiana na radio 5 ili kukuza biashara zao na
kushiriki katika kuendeleza jamii.
Mtangazaji wa kituo hicho Julius Kamafa.
Katika mchakato huo endelevu
utakao fanyika katika jiji la Dar es salaam unataraji kuwapata washindi
wanne wa mkoa huu ambapo washindi hao watajinyakulia zawadi mbalimbali
kama ifuatavyo
Mshindi wa kwanza anataraji zawadi
ya kurekord albam nzima bure kwenye studio za kisasa na kupata
promotion kubwa ya kazi yake,mshindi wa pili anataraji kurekord nyimbo
mbili bure pamoja na pamoja na promotion ya miezi sita(6),mshindi wa
tatu atapata kurekord nyimbo moja pamoja na promotion ya miezi
mitatu,huku mshindi wan ne ataweza kurecord nyimbo moja pamoja na
promotion ya mwezi mmoja.
Msanii Hance Mpozi kutoka Tegeta Dar es Salaam akionesha kipaji chake.
Mashabiki.
Wanii wa kundi moja wakimiliki jukwaa.
Ni Msaga Sumu akitoa burudani.
Mtalamu wa kiduku.
Kulia ni DJ Haazu, pamoja na wasanii.
Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja.
0 comments :
Post a Comment