Nachukua fursa hii kwa masikitiko makubwa sana kutoa Salamu za Rambirambi kwa Familia na Uongozi wa Juu wa Chadema Makao makuu kwa msiba wa Kamanda mwenzetu, Mpiganaji wa kweli, Kijana mwenzetu Ndugu Mohamed Mtoi Kanyawana aliyefariki kwa ajali ya Gari iliyotokea huko Tanga. Kwa kweli bado tulikuwa tunamhitaji sana kamanda mwenzetu lakini kifo ni mpango wa Mungu ametangulia mbele sisi tupo nyuma yake. Tunajua mchango wake wa kujenga Chama na tunauthamini sana. Mohamed Mtoi alikuwa ni tegemeo letu kwenye nafasi ya Ubunge Jimbo la Lushoto pia kama mratibu wa Kanda ya Kaskazini, hivyo tumepata pigo kubwa sana hasa katika kipindi hiki kigumu kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu. Tulikuwa tunashirikiana sana na Ndugu Mohamed Mtoi kwenye kusambaza Taarifa Mbalimbali za Chama, mchango wake ulikuwa mkubwa sana. Mungu aiweke roho ya Marehemu Mohamed Mtoi Kanyawana mahali Pema Peponi.
Picha ya kampeni ya Mohamed Mtoi wakati anagombea Jimbo la Lushoto Tanga
Pichani Gari ambayo ndugu Mohamed Mtoi Kanyawana amepatia ajali akitokea kwenye kampeni
Mohamed Mtoi akiwa na familia yake
Mohamed Mtoi akiwa shule ya msingi 1993
Mohamed Mtoi akiwa kiranja shule ya msingi 1990
Kamanda Mohamed Mtoi akiwa na makamanda wenzake kwenye mkutano mkuu wa Chadema
Kamanda Mohamed Mtoi akiongozana na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe kwenye harakati za kujenga Chama.
Kwa kweli tumempoteza kamanda wa Ukweli kabisa aliyekuwa na mapenzi mema na chama. Mungu akupumzishe mahali pema peponi
Kamanda Mohamed Mtoi akiwa na mtoto wake
Kamanda Moohamedi Mtoi akiwa ziarani barani Ulaya
0 comments :
Post a Comment