- Written by @nkupamah Blog
Rais wa
Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Mhe. Joseph Kabila (wa kwanza kushoto)
pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakitizama
Kikundi cha Ngoma
kilichokuwa kikitoa Burudani kwenye Uwanja wa Ndege, Rais Kabila alikuja
nchini kuhudhuria Sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika hapo jana katika
uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais
Kabila (katikati) akielekea kwenye ndege, kulia ni Balozi Mulamula na
kushoto ni Balozi wa Kongo nchini Mhe. Khalifani Mpango
Mhe. Rais Kabila akipita kwenye gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la wananchi Tanzania.(VICTOR)
Katibu
Mkuu Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiagana na Rais Joseph
Kabila tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini kwake.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula (mwenye pochi mkononi) akiagana na Rais wa Msumbiji
Mhe. Filipe Nyusi
Rais Nyusi akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Shamimu Nyanduga.
Balozi wa
Tanzania nchini Ufaransa ambaye anawakilisha pia nchini Algeria, Mhe.
Begun Taj akimsindikiza Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Algeria, Mhe. Ramtane Lamamra.
Mhe. Lamamra alikuja nchini kwa ajili ya kuhudhiria Sherehe za uapisho
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli.
Mhe. Lamamra akipanda kwenye ndege tayari kabisa kuanza safari ya kurejea nchini Algeria
Picha na Reginald Philip
0 comments :
Post a Comment