Kijue Kilichosababisha TFF Kufuatwa Na TRA Nakuamriwa Kufungwa .

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) leo mchana imelitaka Shirikisho la soka nchini (TFF) kulipa mapato yaliyopatikana wakati Yanga ikicheza na  TP Mazembe mechi ambayo haikuwa na kiingilio.

Mechi hiyo ya kombe la Shirikisho barani Afrika ilichezwa kwenye Uwanja wa Taifa ambapo Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji alitoa ofa kwa mashabiki wote kuingia bure.

Habari ambazo zilipatikana mchana wa leo zilisema kuwa Maofisa wa TRA walifika kwenye ofisi hizo zilizopo Karume na kuamuru watendaji wote kutojihusisha na shughuli yoyote na kila kitu kiachwe ofisini hapo.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kuwa ; “Waliofika hapa ni maofisa wa TRA na walileta nyaraka za kututaka tulipe mapato ya mechi ya Yanga na Mazembe mechi ambayo haikuwa na kiingilio.

“Mbali na hilo kwenye nyaraka zao kumeelezwa mambo mengi ambapo madeni mengine tayari TFF ililipa ingawa wao wanadai kuna faini, hivyo tunashindwa kuelewa TRA wanahitaji nini, nyaraka zipo hapa zimeachwa,” alisema Lucas.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment