Friday, November 13, 2015
@nkupamah blog
Wabunge
wapya kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wanaotarajia kuingia
Bungeni wiki ijayo wametakiwa kupigania kupatikana kwa katiba mpya
itakayowezesha kupatikana kwa tume huru ya taifa ya uchaguzi.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mwenyekiti wa Bavicha wilaya ya Shinyanga mjini
Bw. Samson Ng’wagi amesema kwamba wabunge wa ukawa waliopata nafasi ya
ubunge wanatakiwa kusimamia upatikanaji wa katiba mpya ambayo
itasaidia kuwa na tume huru ya uchaguzi ili kuondoa hali ya sintofahamu
katika chaguzi zijazo kutokana na tathimini ya uchaguzi uliopita.
Ameongeza
kuwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa vijana
hawakuridhishwa na mwenendo mzima wa uchaguzi kwa madai ya kuwepo
hujuma na vitendo vya rushwa kutawala pamoja na vyombo vya dola
kutumika kukisaidia chama tawala ili kiendelee kubaki madarakani..
Kwa
upande wake Katibu wa BAVICHA wilaya ya Shinyanga mjini Zainab Heri
ameitaka Tume ya uchaguzi Zanzibar(ZEC) imtangaze Maalim Seif kuwa
ndiye mshindi wa Urais aliyechaguliwa na wananchi kuliko kufanya
vitendo vinavyoashiria kubaka demokrasia.
0 comments :
Post a Comment