Chadema Iringa yaanza mchakato kumsaka Meya


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Iringa Mjini, kimeanza mchakato wa kumsaka Meya atakayeongoza Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

 
Chama hicho kimesema kuwa kinataka kumtafuta Meya atakayekuwa tofauti na aliyemaliza muda wake kwa kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka.
 
Akizungumza na Nipashe ofisini kwake mjini hapa juzi, Mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Iringa Mjini, Frank Nyalusi,  alisema Chadema kimejipanga kumtafuta Meya mwenye sifa zote za nafasi hiyo ambaye atasimamia makusanyo yote ya halmshauri na miradi yote kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.
 
Nyalusi alisema Chadema itahakikisha inatekeleza ahadi zote zilizotolewa na wagombea wao wa ubunge na udiwani ili wananchi waendelee kuwaamini kwa miaka mingine mitano ijayo.
 
Alisema wataanza na vimbaumbele viwili muhimu ambavyo ni elimu na afya.
 
“Tuliwaahidi wananchi elimu na ndiyo tunayoanza nayo maana wazazi wengi wanashindwa kuwasomesha watoto wao kutokana na michango mingi...Kwenye kampeni zetu za udiwani, ubunge na urais, tulisema elimu itakuwa bure kuanzia darasa la awali hadi chuo kikuu,lakini kwa kuwa tumekosa urais na hatuna Ilani ya Chadema, basi itatubidi tuifuate Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo inasema elimu bure kuanzia kidato cha nne hadi chuo kikuu,” alisema Nyalusi.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment