AJALI:Wanafunzi 18 wamejeruhiwa baada ya bweni kuteketea kwa moto


Wanafunzi 18 Wa Shule Ya Sekondari Philip Mangula Iliyopo Kata Ya Imalinyi Wilayani Wanging’ombe Mkoani Njombe Wamejeruhiwa Katika Ajali Ya Moto Iliyotokea Julai 30 Majira ya saa moja jioni na kuteketeza mali zenye thamani ya milioni 45.
Mtendaji wa kijiji cha Kinenulo Martini Mwalongo amesema kuwa chanzo chamoto huo hakijajulikana na kwamba moto huo umetokea wakati wanafunzi wakifanya ibada katika vyumba vya madarasa huku milango na madirisha katika mabweni yaliyo ungua vikiwa yamefungwa.
Baadhi ya wanafunzi wameiambia ITV kuwa mabweni yaliyoungua ni matatu yote yakiwa ni ya wavulana huku wazazi wakiiomba serikali kuhakikisha chanzo cha moto huo kinafahamika haraka.
Katibu tawala wa mkoa wa Njombe Jackson Saitabau amefika shule ya sekondari Philip Mangula mapema asubuhi na kuagiza wanafunzi kuendelea na masomo na kwamba halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wakiendelea kufanya tathmini ya mali zilizoungua na vikiwemo vifaa vya Wanafunzi.
Chanzo ITV Tanzania
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment