Na K-Vis Media
UONGOZI wa Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere unaomilikiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania, TAA, umetangaza leo Ijumaa Novemba 27, 2015 kuwa kuanzia sasa
vifurushi na mizigo mingine yote ya Shirika la Posta Tanzania,
itakaguliwa kwa mara ya pili kama mizigo mingine yoyote kabla ya
kupakiwa ndani ya ndege.
Uamuzi huo umetangazwa na
Mkurugenzi wa Uwanja huo, (JNIA), Injinia Thomas Haule, wakati
akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
mikutano wa VIP ulioko uwanjani hapo.
Alisema, uamuzi huo ni baada ya
Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege, TAA, kutoa maonyo kadhaa, kwa Shirika la
Posta, kuimarisha ukaguzi wa vifurushi na mizigo itokayo Posta kwa vile
imekuwa ikikamatwa na mizigo ambayo ni tofauti na iliyokusudiwa.
Alitaja mizigo hiyo kuwa ni pamoja
nabangi, na kwamba, Uholanzi wamekuwa wakilalamika mara kadhaa kuwa
wamekuwa wakikamata vifurushi vya Posta vikiwa na mizigo
iliyoharamishwa.
“Sisi Kama Mamlaka, wajibu wetu
mkubwa ni kuzuia kitu au vitu vyovyote vinavyoweza kuhatarisha usalama
wa abiria wawapo ndani ya ndege au ndege yenyewe haviingii ndani ya
ndege.” Alianza kwa kusema Injinia Haule na kuongeza kuwa, vitu vingine
kama madawa ya kulevya, pembe za ndovu, na vingine vingi, ,
vinashughulikiwa na mamlaka nyingine ambazo zina maafisa wake hapa JNIA
wakishirikiana na maafisa wetu.
Hata hivyo makosa yafanywayo na
idara Fulani ya serikali yenye afisa wake hapa JNIA, ni wazi kwamba
watakaonyooshewankidole ni TAA, alisema na kubainisha kuwa Mamlaka
haitavumilia tena uzembe utakaofanywa na taasisi nyingine ya serikali
katika kuhakikisha zinatekeleza wajibu wake ipasavyo


0 comments :
Post a Comment