Saturday, November 14, 2015
@nkupamah blog
MBUNGE
mteule wa Mikumi kupita Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Joseph Haule aka Profesa Jay, amemtaka Rais John Magufuli kumteua msanii
mmoja kuwa mbunge katika nafasi zake 10, ili akawakilishe kundi wasanii
bungeni.
Profesa
Jay, ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, amesema kuwa Rais
anapaswa kufanya hayo kwa vile serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
imewatumia wasanii hao katika harakati zake za kuingia madarakani.
Akizunguza na wandishi wa habari nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana,
Profesa Jay, amesema kuwa Rais anapaswa kutambua umuhimu wa wasanii hao
badala ya kuwatumia katika mambo mbalimbali ya kisiasa kisha
kuwatelekeza.
“Wanasiasa wamekuwa wakiwatumia sana wasanii wakati wa kampeni lakini wakimaliza wasanii husahaulika kabisa,” amesema Prof. Jay.
Akizungumzia
mpasuko kati ya wasanii ambao walikuwa wakishabikia chama tawala na
kuchukia vyama pinzani, amesema hana kinyongo nao kwani kila mtu alikuwa
na mapenzi yake lakini anashukuru kuwa wako waliyomuunga mkono japo
walikuwa wakishabikia CCM, ambapo aliwatajana majina kuwa ni Mwinjuma
Hamisi (Mwana F), na Judith Wambura (Lady Jay Dee).
Prof.
Jay, amesema wapo baadhi ya wasanii ambao walidhani kuwa kuingia
bungeni ni jambo ambalo haliwezekani kwa msanii hususani kupitia katika
chama cha upinzani.
“Mimi
nimewasamehe wasanii wote jambo hawakuwa katika upande wake lakini pia
nawapongeza wale wote ambao walikuwa na mimi cha msingi sasa tuungane na
tufanye kazi,” amesema.
Mbali
na hilo Prof. Jay amesema licha ya yeye kuwa mbunge wa jimbo la Mikumi
kamwe hawezi kuachana na fani yake ya mziki kwa kuwa fani hiyo ni sehemu
ya mafundisho kwa jamii.
Kuhusu
kuchaguliwa kwake kuwa mbunge Prof. Jay amesema yeye ni mbunge wa jimbo
ambapo anatakiwa kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi za vyama
vya siasa wala dini.
“Kwa
sasa ninayo kazi moja ya kuhakikisha ninavunja makundi ninajua kwa sasa
yapo makundi mengi kutokana na uchaguzi lakini jambo pekee ni kuvunja
makundi kwa lengo la kuwapatia maendeleo wananchi,” anasema Prof. Jay.
Prof.
Jay amesema hakuna haja ya makundi hayo kuendelea kuwepo, kwani
kinachotakiwa hivi sasa ni watu Wanamikumi kutumia fulsa zote kwa ajili
ya kujisogezea maendeleo huku wakikumbuka kuwa maendeleo hayana itikadi.
“Sina
sababu ya kuendeleza makundi, wana Mikuni walikuwa kama wakiwa katika
jimbo lao lakini kwa sasa kinachotakiwa ni kuhakikisha wanapata
maendeleo hususani katika sekta ya afya,” alisema Prof. Jay.
0 comments :
Post a Comment