Monday, November 30, 2015
@nkupamah blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.
Tayari
fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa
barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo,
linalopaswa kuanza mara moja
Akizungumza
na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar
es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka
ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika barabara hiyo
Kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.
Wakati
huo huo, Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba
Ikulu Jijini Dar es salaam.
Katika
Mazungumzo hayo Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa
kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia
kwa kutoa hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania iliyokonga nyoyo za Watanzania.
Kwa
Upande wake Rais Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake
thabiti wa kupinga ufisadi na amemtakia heri katika shughuli zake.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.
30 Novemba,2015
0 comments :
Post a Comment