Wahakumiwa Miaka 30 Jela Kwa Kumuibia Jaji wa Mahakama Kuu

Wednesday, November 25, 2015

  @nkupamah blog
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu kwenda jela miaka 30 watu wanne baada ya kukutwa na hatia ya makosa kula njama, uporaji na unyang’anyi wa kutumia silaha vitu vyenye thamani ya Sh. milioni 15 mali ya Jaji John Mgeta, wa Mahakama Kuu Tanzania.
 
Waliopewa adhabu hiyo ni wafanyabiashara James Warioba (29) maarufu kama Sailensa, Abdulkarim Hussein ama Muddy, Seif Lusonzo ama Dege, Ally Mdege, Lusekelo Mundengese ama Tekero, Omary Hassan na mlinzi Benjamin Macklin, wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
 
Hukumu hiyo ilisomwa jana na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Devotha Kisoka.
 
Alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 12 wa upande wa Jamhuri bila kuacha shaka, Mahakama imewatia washtakiwa hatiani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment