DAR ES SALAAM
Mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake
mara moja aliejifanya Afisa wa mamlaka ya mapato – TRA aliyekuwa na gari
lenye namba za usajili T945 BYG amenusurika kifo mara baada ya kula
kichapo
kutoka kwa wananchi wakati akiwa kwenye harakati za kufanya
utapeli kwenye duka kubwa la VEW POINT lililopo Tabata Segerea jijini
Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa wafanyakazi wa duka hilo
mtu huyo aliejifanya afisa kutoka mamlaka ya mapato TRA sio mara ya
kwanza kufika eneo hilo kwani siku moja kabla alifika akiwa na wenzake
wawili na mmoja waliyemtambulisha kuwa ni mwandishi wa habari na
kufanikiwa kutapeli kiasi cha shilingi milioni tano.
Mtuhumiwa huyo sasa amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Tabata Segerea kwa hatua zaidi za Kisheria.
0 comments :
Post a Comment