Afisa Wa Jeshi la Polisi Ajinyonga

Nkupamah media

Afisa wa Polisi Mkoani Arusha aliyetajwa kama PC Halfani, alikutwa akiwa amejinyonga katika eneo la kambi ya makazi ya askari wa jeshi la polisi jijini humo jumapili iliyopita.
Askari huyo ambaye alikuwa anahusika na ulinzi wa kutumia polisi na farasi alikutwa na wakazi wa eneo hilo akiwa amening’ing’inia juu ya mti huku sababu za kujitoa roho kwa hali ya kusikitisha zikiwa kitendawili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa ARusha, Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo japo alikataa kutoa maelezo kuhusu tukio hilo akidai kuwa hilo ni tukio lisilopaswa kutolewa maelezo kwa umma.
“Mambo yanayohusiana na polisi hayapaswi kwenda kwenye vyombo vya habari,” alisema Liberatus Sabas.
Wakazi wa eneo hilo la makazi ya polisi walitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu kabla haujasafirishwa kwenda mkoani Singida kwa ajili ya mazishi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment