Mbunge
wa Mafinga mjini Cosato Chumi akikagua chanzo maji cha ikangafu wakati
wa ziara yake ya kutembelea vyanzo vya maji na
matanki ya kuhifadhia
maji
Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi akikagua moja ya tanki la kuhifadhia maji
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya mji wa Mafinga Shaibu Nnunduma kulia akiwa mbunge
Cosato Chumi wakijadili jambo kwenye moja ya matanki waliyokuwa
wanayakagua.
Kushoto
ni Bw Uhaula ,Bw. Shaibu Nnunduma Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa
Mafinga wakijadili jambo baada ya kukagua baadi ya vyanzo hivyo vya
maji.
Mbunge
wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi amefanya ziara ya kuangalia
jinsi gani anaweza kutatua tatizo la maji katika jimbo hilo.
Leo
mapema mbunge huyo aliongozana na wataalamu wa maji na mkurugenzi wa
maji wa Mafinga walifanya ziara kwenye vyanzo vya maji kwa lengo la
kutatua tatizo la maji ambalo limedumu kwa kipindi kirefu.
Akizungumza
katika ziara hiyo Chumi amesema kuwa ameamua kufanya ziara katika eneo
hilo kwa lengo la kujua nini tatizo linalosababisha miji wa Mafinga kuwa
na uhaba wa maji.
“Huwezi
kutatua tatizo bila kulijua tatizo lenyewe hivyo nimelazimika kufanya
ziara na kufika huku ili nijionee mwenyewe nini tatizo na nianze
kuangalia na kupanga mikakati ya kulitatua tatizo hilo ambalo limekuwa
sugu katika mji huo” alisema Chumi
Aidha Mh. Chumi alisema kuwa mji wa Mafinga unahitaji maendeleo hivyo moja ya mambo yanayosababisha maendeleo ni maji hivyo ni lazima kulitatua tatizo hilo mapema ili wananchi waendelee kufanya kazi na kuacha kulifikiria tatizo hilo ambalo limekuwa likiwagharimu muda mwingi wa kwenda kutafuta maji.
Aidha Mh. Chumi alisema kuwa mji wa Mafinga unahitaji maendeleo hivyo moja ya mambo yanayosababisha maendeleo ni maji hivyo ni lazima kulitatua tatizo hilo mapema ili wananchi waendelee kufanya kazi na kuacha kulifikiria tatizo hilo ambalo limekuwa likiwagharimu muda mwingi wa kwenda kutafuta maji.
“Leo
nimekuja na wataalamu wa maji wa mji wa Mafinga ili wanieleze nini
tatizo kitaalamu na tutumie njia gani kulitatua tatizo hilo ndio maana
unaniona nipo na hawa wataalm lengo langu ni kulimaliza kabisa tatizo la
maji katika mji huu wa Mafinga” alisema chumi
Pia
chumi amewahakikishia wananchi wa jimbo la Mafinga mjini kuwa
atahakikisha anatatua tatizo hilo kwa kuwa ili kuwa moja ya sera yake
wakati wa kuomba kura kwa wananchi hivyo lazima atimize ahadi
aliyoihaidi.Chumi amemalizia kwa kuwaomba wananchi wa jimbo hilo kumpa ushirikiano kwa jambo lolote lile analolifanya la maendeleo katika jimbo hilo na kuwaomba wawe na subira wakati anapanga mikakati ya kutengeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kuomba kura.
0 comments :
Post a Comment