Abiria 2 wakamatwa Paris
Maafisa
wa polisi nchini Ufaransa wamewatia mbaroni mume na mkewe waliokuwa
abiria katika ndege ya Air France iliyolazimika kutua kwa dharura nchini
Kenya hapo jana kufuatia tishio la bomu ikiwa angani.
Duru
zinasema kuwa wawili hao ambao majina yao bado hayajatangazwa hadharani
walikamatwa punde baada ya kutua katika uwanja wa kimataifa wa Charles
de Gaulle.- Yamkini waliokamatwa ni afisa mmoja mstaafu wa polisi ambaye ni mshukiwa mkuu huku mkewe akitumika kama shahidi.
- Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air France alifutilia mbali tahadhari ya' bomu' iliyosababisha ndege ya kutua Kenya kuwa ni bandia.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria 459 na wahudumu 14.
Frederic
Gagey aliwaambia waandishi wa habari mjini Paris Ufaransa kuwa kifaa
kilichodhaniwa kuwa kilipuzi kilikuwa ni mbao na kisanduku cha karatasi
tu wala hakikuwa na uwezo wowote wa kuhatarisha usalama wa ndege hiyo.
Ndege
hiyo ya Ufaransa chapa Boeing 777 nambari AF463 inayohudumu kati ya
Mauritius na Paris ililazimika kutua baada ya kile kinachotajwa kuwa
bomu bandia.
Inasemekana kuwa abiria mmoja alikipata kifaa hicho chooni na akamfahamisha mhudumu mmoja wa ndege hiyo.
- Ndege hiyo ilikuwa na abiria 459 na wahudumu 14.
Mume na mkewe wamekamatwa walipotua mjini Paris
Mhudumu huyo alimfahamisha rubani kuhusiana na kifaa hicho na shughuli za kutua kwa dharura zikaanza.
Ndege
hiyo ilitua saa sita usiku wa kuamkia Jumapili, huku wataalamu wa
kutegua mabomu kutoka jeshi la wanamaji la Kenya wakiingia ndani ya
ndege hiyo kukagua kifurushi kilicholeta taharuki.
Sasa kitengo cha ujasusi cha Ufaransa kimeanzisha uchunguzi wa kina kubaini kilichosababisha tishio hilo.BBC
0 comments :
Post a Comment