MC WA MISS UNIVERSE AJICHANGANYA NA KUMTAJA MSHINDI AMBAYE HAKUSTAHILI(VIDEO NA PICHAZZ)


Nkupamah media


KATIKA hali isiyo ya kawaida Mshereheshaji katika kinyang’anyiro cha kuwania taji la Miss Universe Steve Harvey alijikuta akimpa wakati mgumu Miss Colombia mara baada ya kutangaza kuwa alikosea kumtangaza mshindi wa taji hilo.2F8A9E1600000578-3368439-image-a-44_1450669166760Katika tukio hilo ambalo limewaacha watu wengi vinywa wazi,lilishuhudia Steve akimtaka radhi Miss Colombia na kumtangaza Miss Uphilipino kuwa ndiye aliyekuwa anastahiki kushinda taji hilo kwa mujibu wa karatasi aliyokuwa nayo ya matokeo ya mwisho.2F8ABBBB00000578-3368439-image-a-119_1450672680518Hata hivyo haikumwia vigumu Miss Colombia kuvua taji hilo ambalo alikaa nalo kwa muda usiozidi dakika tano kabla ya matokeo ya awali kubadilishwa wakati akiwa katika harakati za kusherekea ushindi huo.2F8ABC3700000578-3368439-image-a-123_1450672707632Muda mfupi mara baada ya kuvuliwa taji hilo huku akiwa ameshika bendera ya taifa lake alijikuta akitokwa na machozi mithili ya mvua hali iliyowapa wakati mgumu washiriki wenzake na Steve kumbembeleza .
Hata hivyo Steve alikata mzizi wa fitina mara baada ya kuanika hadharani matokeo yaliyoandikwa katika kikaratasi cha kutangaza matokeo ambacho pia kilionyesha kuwa Miss Uphilipino ndiye alikuwa mshindi2F8AA27000000578-3368439-image-a-62_1450669736797
Je Ungekuwa ndiyo wewe ungefanyaje
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment