Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa
la Ujenzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akizungumza na waandishi wa
habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu Baraza hilo lilivyofanikiwa
kutatua migogoro
kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi Mhandisi Dkt.
Leonard Chamuriho leo Jijini Dar es salaam kuhusu Baraza hilo
lilivyofanikiwa kutatua migogoro kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya
Ujenzi nchini.
……………………………………………………………………………………………………
Frank Mvungi- Maelezo
Baraza la Taifa la Ujenzi
limepokea migogoro 41 na kufanikiwa kuitafutia ufumbuzi katika kipindi
cha mwaka 2015 kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu
wa Baraza la Taifa la Ujenzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho wakati wa
mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.
Akizungumzia majukumu ya Baraza
hilo katika kutatua Migogoro inayojitokeza katika Sekta hiyo, Mhandisi
Chamuriho amebainisha kuwa migogogoro iliyojitokeza imekuwa ikitegemea
Ukubwa wa mradi, Hali ya eneo la mradi, Ubora wa kazi, uelewa wa
vipengele mbalimbali vya mkataba katika mradi husika na moja ya pande
zinazohusika kukatisha mkataba.
Kakika kukabiliana na migogoro
hiyo, Baraza hilo limekuwa likitumia njia mbalimbali ikiwemo kutoa
ushauri wa kitaalamu kwa pande zinazohusika katika mradi, kuwakutanisha
wadau chini ya Baraza, kuweka wahusika chini ya aliyetatua mgogoro
husika.
Akifafanua, Mhandisi Dkt.
Chamuriho amebainisha kuwa Baraza hilo limekuwa likitumia njia hizo
kutatua Migogoro katika sekta hiyo pale inaposhindikana wahusika
wanaweza kwenda mahakamani kama hatua ya mwisho katika kutatua mgogoro
husika.
Pia alitoa wito kwa watanzania
wote hasa wadau wa Sekta ya Ujenzi kuwa na uelewa mzuri wa jinsi ya
kutekeleza miradi ya ujenzi kwa kuzingatia Sheria na kanuni ili kuepuka
Migogoro.
Baraza la Taifa la Ujenzi ni
Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge namba 20
ya mwaka 1987 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2008.(National
Construction Council Act, CAP 162,R.E.2008) ambapo Baraza lilianza
kufanya kazi tarehe 17 August 1981.
0 comments :
Post a Comment