Diamond
Platnumz akiwasalimia mashabiki wake waliofurika katika eneo la Karume
leo kwenye mkutano na wanahabari kuhusu shoo yake itakayofanyika Dar
Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda sambamba na mashabiki waliofurika Karume leo.
Mashabiki wakiwa wamepagawa wakati Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
Meneja
Masoko wa Global Publishers na Dar Live, Innocent Mafuru (mwenye
tisheti nyeupe aliyesimama kulia) akiwakaribisha wanahabari, wasanii na
mashabiki wa burudani katika mkutano na wanahabari kuelekea shoo ya
Funga Mwaka itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho akielezea jinsi walivyojipanga kwa shoo hiyo ya Krismasi.
Mratibu
wa Burudani Dar Live, Juma Mbizo akiongea na wanahabari pamoja na
mashabiki (hawapo pichani) kuhusu walivyojipanga kuwapa burudani
mashabiki siku ya Krismasi.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Staric ambaye naye atapanda jukwaani siku hiyo akiongea na mashabiki.
Diamond akizidi kuwapagawisha mashabiki wake.
Baada ya kuongea na mashabiki wake Diamond aliamua kugawa CD na DVD za nyimbo zake kwa mashabiki waliohudhuria.
Diamond akiwaaga mashabiki na kuwataka wakutane Dar Live katika Sikukuu ya Krismasi.
Mashabiki wakiwa wamemzingira Diamond wakati akiondoka eneo la mkutano na wanahabari leo.
STAA
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaahidi shoo ya nguvu
mashabiki wake na kuwataka waje kwa wingi katika shoo kali ya kufunga
mwaka itakayopigwa Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar katika Sikukuu ya X-mas
na kuwa hatawaangusha.
Diamond
anayetamba na ngoma ya Utanipenda ameyaongea hayo leo kwenye mkutano
maalum uliofanyika Karume, Dar ambao ulihusisha waandishi wa habari na
wapenzi wa muziki kwa ajili ya kuzungumzia shoo hiyo kubwa kuliko
inayojulikana kama Funga Mwaka Concert.
“Itakuwa
ni Sikukuu ya Krismasi, sasa kwa nini tusifurahi pamoja, kama MTV
wameamua kunipa tuzo ya Mtumbuizaji Bora Afrika kwa hiyo sihitaji
kuongea sana shoo itakuwaje siku hiyo, naomba mje kwa wingi kwa kweli
sipendi kuwaudhi, nawaahidi sitawaangusha,” alisema Diamond au Baba
Tiffah.
Pia
waandaji wakuu wa shoo hiyo, Global Publishers Ltd, kupitia kwa Meneja
Mkuu, Abdallah Mrisho, naye alizungumza machache pamoja na kutambulisha
listi ya wasanii wengine watakaoambatana na Diamond siku hiyo.
“Mbali
na Diamond pia kutakuwa na Msagasumu, Wakali Dancers, Staric pamoja na
burudani nyingine nyingi.
Haitakuwa shoo ndogo, Diamond ameamua kufurahi na mashabiki wa muziki
siku ya Krismasi kwa kufunga na kuukaribisha mwaka mpya. Shoo zitaanza
asubuhi kwa watoto mpaka saa 12 jioni kisha baada ya hapo ni watu wazima
mpaka alfajiri,” alisema Mrisho.
Viingilio
ni Sh 15,000 na kwa V.I.P ni Sh 30,000 lakini wadhamini wakuu wa shoo
hiyo, Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel wakaamua kutoa ofa ya punguzo la
bei kwa tiketi 1,000 za awali kwa watakaokata kupitia kadi mpya za
Airtel Money Tap Tap zenye mfumo mpya wa kulipia bili mbalimbali.
“Kadi
za Tap Tap zinazorahisisha kufanya malipo zaidi popote ulipo bila ya
gharama yoyote tayari zipo zinapatikana maeneo ya Temeke na Ilala lakini
kuwa nayo unapaswa kuwa na kadi ya Airtel na kwa wateja 1,000 wa kwanza
wenye Tap Tap watakaokata tiketi kupitia kadi hiyo watakuwa na punguzo
la Sh 5,000 yaani kwa 15,000 itakuwa 10,000 na 30,000 itakuwa 25,000,”
alisema Meneja Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane Matinde.
0 comments :
Post a Comment