Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw.
Said Meck Sadick akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani ofisini
kwake leo alipokutana nao kuelezea utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa
kwa
DAWASCO kuhusu usambazaji wa maji safi na salama ili kukabiliana na
mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO
Mhandisi Cyprian Luhemeja akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani
Dar es salaam leo alipokutana nao kuelezea utekelezaji wa maagizo
yaliyotolewa na Serikali kuhusu usambazaji wa maji safi na salama ili
kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Picha zote na Ally Daud-Maelezo
……………………………………………………………………………………………………………
NA ALLY DAUD-MAELEZO
Shirika la Maji Safi na Maji Taka
Dar es salaam (DAWASCO) limeongeza uzalishaji na usambazaji wa Maji
safi na Salama kwa wakazi wa jiji hilo hadi kufikia mita za ujazo
280,000 kwa siku ili kubabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu
uliolikumba jiji hilo hivi karibuni.
Hatua hiyo inatokana na
utekelezaji wa maagizo ya Serikali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Said Meck Sadiki kuitaka DAWASCO kusambaza maji safi na salama
kwa wakazi wa jiji hilo ili kupambana na Ugonjwa wa Kipindupindu.
Akiongea na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam Mkuu wa mkoa huo Bw. Sadick amesema kuwa
kufuatia maagizo aliyoyatoa kwa shirika hilo ikiwemo kusambaza maji safi
na salama kwa wananchi pamoja na kutengeneza mifereji ya kupitsha maji
taka ili yasiingiliane na mikondo ya maji safi, DAWASCO wametekeleza kwa
kiasi kikubwa maagizo hayo.
“Dawasco imehakikisha inazalisha
maji safi na salama kati ya mita za ujazo 270,000 na 280,000 kila siku
kwa muda wote tangu mlipuko ulipotokea na imehakikisha inasafisha na
kusambaza kwa wananchi yakiwa katika viwango vya ubora unaokubalika kwa
ajili ya matumizi kwa binadamu” amesema Bw. Sadick.
Ameongeza kuwa Dawasco imejenga
vizimba vya maji safi na salama kwenye maeneo mbalimbali ambayo
hayajakumbwa na yaliyokumbwa na athari za mlipuko wa ugonjwa huo kwa
jumla ya vizimba 48 ambavyo maeneo ya Kinondoni vizimba 5, Magomeni
vizimba 38 na Ilala vizimba 5.
Aidha, amesema kuwa DAWASCO kwa
kushirikiana na Ofisi ya Bonde Wami Ruvu imeanza kazi ya kusajili na
kuwatambua watu binafsi wenye visima virefu vilivyopo kisheria ambao
wanauza maji kwa wananchi ili kuvitambua na kudhibiti ubora wa maji na
bei yake ambapo zoezi hili litaendelea hadi Machi 2016.
“Dawasco imefanya jitihada za
kuweka dawa ya kuua wadudu aina ya chrolination kwenye maboza wakati
wa usajili kabla ya kuruhusiwa kufanya biashara ya kuuza maji kwa
wananchi na kuongeza sehemu za kuchota maji kwa kuwapelekea wananchi
huduma hiyo wakitumia magari yenye matanki yaliyokuwepo kutoka 12 mpaka
kufika 49 kwa sasa” aliongeza Bw.Sadick.
Katika hatua nyingine Bw. Sadick
alitoa rai kwa wakazi wa jiji hilo kuendelea na tabia ya kufanya usafi
mara kwa mara ili kutokomezakabisa ugonjwa wa kipindupindu kwani kuanzia
juzi hakuna wagonjwa waliopokelewa katika vituo vyote.
Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu
wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema kuwa wako katika hatua za
mwisho kukamilisha ujenzi wa mifereji ya kupitisha maji machafu ili
isiingiliane na maji safi kwa wiki mbili zijazo.
“kufikia Februari mwakani
tutaweza kutoa maji safi na salama ya kutosha kwa wananchi wote wa Dar
es salaam bila ya matatizo yoyote” alisisitiza Mhandisi Cyprian.
0 comments :
Post a Comment