RC Makalla azindua mradi wa maji wenye thamani ya sh Milioni 343 kijiji cha Mabogini, mkoani Kilimanjaro

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makalla mwenye miwani akizindua huduma ya maji katika kijiji cha Mabogini, mkoani Kilimanjaro wenye thamani ya Sh Milioni 343.

………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu,
Kilimanjaro
ZAIDI ya wananchi 3000
wa kijiji cha Mabogini, kitongoji cha Shabaha, mkoani Kilimanjaro, watanufaika
na huduma ya maji safi na salama, baada ya kupelekewa mradi wenye thamani ya Sh
Milioni 343.
Mradi huo
uliozinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, umesimamiwa na
Mamlaka ya Maji Safi Moshi (MUASA), ukiwa na lengo la kuwapatia huduma bora ya
maji wakazi katika kijiji hicho.
 
Akizungumza katika
uzinduzi huo, RC Makalla aliwataka wananchi kutunza mazingira na kulinda vyanzo
vya maji, bila kusahau upandaji wa miti ili wasiharibu vyanzo vya maji.
Alisema bila hivyo
hali ya maji katika maeneo hayo itakuwa ngumu, hivyo kuna kila sababu ya
wananchi hao kuielewa na kuiabudu sera ya utunzaji wa
mazingira na upandaji wa miti katika maeneo
yao.
“Naomba wananchi
tulinde miundo mbinu ya maji ili kuhakikisha kwamba miradi ya maji inakuwa
endelevu katika maeneo yetu tunayoishi, maana maji ni uhai.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla akimtwishwa ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Mabogini baada ya uzinduzi wa mradi maji katika eneo hilo.
Mazungumzo yanaendelea katika uzinduzi huo wa maji.
RC Kilimanjaro Amos Makalla akifungua maji kama ishara ya kuzindua rasmi mradi huo.
RC Kilimanjaro Amos Makalla wa nne kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali mkoani Kilimanjaro na watendaji wa MUASA.
 
“Tunaamini tukiamua kwa pamoja kufuata maelekezo ya wataalaamu juu ya utunzaji wa mazingira tutaishi vizuri na huduma ya maji itapatikana kwa urahisi,” alisema RC Makalla.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amekabidhi hundi yenye thamani ya Sh Milioni 100 kwa vikundi 45 kwa Halmashauri ya Moshi, huku vikundi hivyo vikiwa ni 39 vya akina mama na 6 kwa vijana. Fedha hizo ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali kwa Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kutoa mikopo kwa akina mama na vijana.
 
RC Makalla ni miongoni mwa viongozi wa serikali wanaokwenda na kasi ya Hapa Kazi Tu inayoendeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli, akisimamia na kuzunguuka katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kufanikisha maendeleo ya wananchi wake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment