SOMALIA
Serikali ya Somalia imepiga marufuku sherehe za kuadhimisha sikukuu ya Krismasi katika mji mkuu wa Mogadishu.
Mkurugenzi mkuu katika wizara ya maswala
ya dini,Sheikh Mohamed Khayrow, ameonya kuwa
maadhimisho kama hayo
yasiyofungamana na dini ya kiislamu yanaweza kusababisha mashambulizi ya
kundi la wanamgambo wa Al Shabab.
”Maafisa wote wa kulinda
usalama wanapaswa kusimamisha ama kuvunja mikutano ya aina yeyote yenye
nia ya kuadhimisha sikukuu hiyo isiofungamana na dini ya Kiislamu.” alisema Sheikh Mohamed
Mwaka uliopita wapiganaji wa Al shabab
walishambulia kambi ya majeshi ya muungano wa Afrika AU iliyoko
mogadishu wakati wanajeshi hao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya
Krismasi.
Wanajeshi 5 waliuawa katika shambulizi hilo la kunyemelea,Asilimia kubwa ya raia wa Somalia ni wasilamu.
0 comments :
Post a Comment