DAR ES SALAAM
KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo
Zitto Kabwe ameelezwa kufurahishwa na jitihada za kumaliza mzozo wa
kisiasa visiwani Zanzibar,huku akitaja baadhi ya mbinu ambazo chama
chake waliishauri Serikali
ambazo zimeanza kuchukuliwa hatua.
Hii hapa chini ni post yake katika mtandao wa facebook juu ya suala hilo
Zanzibar tartiibu….
Disemba 20 mwaka huu 2015 Kamati ya Uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo ilitoa tamko lake baada ya kufuatilia hali ya Zanzibar.
Moja ya
mambo yaliyoelezwa katika tamko hilo ni uwepo wa askari wengi katika
kisiwa hicho hali iliyokuwa inatishia amani kwa wananchi
Taarifa
hiyo ya ACT mbali na masuala mengine, ikaeleza kuwa ni wakati muafaka
kwa serikali kuhakikisha inawarudisha askari hao wa vikosi mbali mbali
kuanzia jeshi la Polisi,JKU,KMKM JWTZ na Mafunzo katika makambi yao.
Lengo
likiwa ni kuwaacha wananchi wakiwa katika uhuru wa kufanya shughuli zao
wakati suala la mtanziko wa kisiasa kisiwani humo ukiwa unafanyiwa kazi
Kuanzia
jana Disemba 22 na leo Disemba 23 majeshi hayo yameshaanza kuondoka
katika maeneo mbali mbali ya mji wa Znz hali inayoashiria mwanzo wa
mwisho mwema katika kadhia ya uchaguzi wa Zanzibar.
Ninaomba mamlaka husika ziendelee kufanyia kazi mapendekezo yetu mengine ili kulimaliza kabisa suala hili.
0 comments :
Post a Comment