Taswira ya baadhi ya mitaa ya katikati ya Kariakoo, Dar ilivyofurika umati wa watu.
Harakati za hapa na pale zikiendelea katika mitaa ya Msimbazi, Kariakoo.
Baadhi ya wakazi wa Dar wakichangamkia kununua nguo za sikukuu kwenye mitaa ya Kongo na Msimbazi.
Barabara ya Msimbazi ambayo imejengwa na kampuni ya ujenzi ya Strabag ilivyoonekana kufurika watu kwa kuuzia bidhaa chini.
Harakati zikiendelea katika barabara ya Msimbazi, Kariakoo.
Hali halisi ya maeneo ya mitaa ya Kariakoo ilivyokuwa kila mahali.
ZIKIWA
zimebaki siku mbili waumini wa dini ya Kikristo duniani kusherehekea
sikukuu ya Krismas ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, baadhi ya wakazi wa jiji
la Dar es Salaam, jana kwa wingi wao, wameonekana wakifanya manunuzi ya
nguo na bidhaa mbalimbali za sikukuu katika mitaa ya Kariakoo.
Kamera
yetu imefanikiwa kunasa baadhi ya picha zinazoonesha wakazi wa jiji la
Dar es Salaam, wakiwa katika shamrashamra za manunuzi na kusababisha
mitaa kutokupitika kwa urahisi kutokana na msongamano wa watu.


0 comments :
Post a Comment