DAR ES SALAAM
RAIS John Magufuli amekutana na kufanya
mazungumzo na Spika wa Seneti na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Burundi,
Reverien Ndikuriyo Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya kisiasa na
usalama nchini Burundi
na jitihada zinazochukuliwa na Tanzania, ikiwa ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Akiwasilisha ujumbe wa Rais Pierre
Nkurunziza wa Burundi kuhusu hali ya Burundi, Spika Ndikuriyo alisema
Serikali ya Burundi ipo tayari kufanya mazungumzo na wadau wote wa siasa
kuhusu hali ya nchi hiyo na jitihada za kuumaliza mgogoro wa kisiasa
unaoendelea nchini humo.
Akitoa maelezo ya kikao hicho kwa niaba
ya Dk Magufuli, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk Augustine Mahiga alisema Serikali ya
Burundi imekubali usuluhishi, unaofanywa na Rais Yoweri Museveni wa
Uganda kwa niaba ya Marais wa EAC kutokana na kikao kilichofanyika Dar
es Salaam Julai mwaka huu na kwamba Serikali ya Burundi iko tayari
kushiriki mazungumzo hayo ya amani.
“Nimeagizwa nipeleke taarifa
kwa mawaziri wa nchi za nje wa nchi jirani juu ya maandalizi ya
mazungumzo hayo ambayo yataanza kule Uganda tarehe 28 mwezi Desemba”, alisema
0 comments :
Post a Comment