Tumekuwa tukisikia watu wanafungwa kwa kutakatisha fedha, wengine kuhujumu uchumi, sasa leo tumempata mtaalamu kutoka Bank Kuu ya Tanzania (BoT), Meneja Msaidizi Idara ya Uendeshaji kesi na uchunguzi Ganga Mlipano kwenye huu ufafanuzi.
“Nchi yoyote inatakiwa kuwa na uchumi imara vitendo vyovyote vinavyofanya uchumi usiwe imara ni vitendo vinavyofanya uchumi uhujumiwe ndio maana Serikali yetu ilitunga sheria ya uhujumu uchumi mwaka 1984.
“Vitendo vyote vinavyofanywa ambavyo vimeelezewa kwenye hiyo sheria vinavyopelekea kuhujumu uchumi vinaitwa vitendo vya kuhujumu uchumi na mtu yeyote akifanya hivyo vitendo anapelekwa Mahakamani na kushtakiwa.
“Ili uchumi uendelee lazima kuwe na mtiririko wa fedha, mtu anapochukua fedha akaweka nyumbani au akachukua bidhaa nyingi za kiasi kikubwa akazihifadhi nyumbani na wananchi wakakosa maana yake kutatokea mfumuko wa bei. Vitendo kama hivyo ndio hupelekea uchumi uyumbe.
“Vitendo vinavyopelekea masuala haya ndio vinaitwa vitendo vya kuhujumu uchumi. Na hukusu kutakatisha fedha…fedha kwa kawaida inatakiwa kutumika kama ilivyopangwa. Mtu anaweza kupata fedha kwa njia sio ya halali na akaitakatisha…” – Ganga Mlipano.
0 comments :
Post a Comment