Rais Magufuli Awatakia Heri Watanzania Wote Katika Siku ya UKIMWI Duniani.

Tuesday, December 1, 2015

  @nkupamah blog

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika siku ya UKIMWI duniani itakayofanyika kesho tarehe 01 Desemba, 2015

Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema jukumu la kupamana na UKIMWI linamhusu kila mtu na hivyo amewasihi watanzania kuzingatia mahubiri ya viongozi wa dini, na pia kuzingatia elimu itolewayo na wataalamu wa afya katika kujikinga na ugonjwa huo.

Dkt. Magufuli amewahakikishia waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI kuwa Serikali itaendelea kuimarisha tiba na huduma zao na ndio maana alielekeza fedha zote zilizopatikana kwa kufuta shamrashamra za maadhimisho hayo zielekezwe kununulia dawa za kurefusha maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI.

Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa elimu kwa umma juu ya kuepukana na maambukizi mapya na kuhimiza watu kujitokeza kwa hiari kupima afya zao.

Amewaomba viongozi katika ngazi zote kuendelea kuwahimiza akinamama wajawazito kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kuchunguza afya zao ili wale ambao watakaogundulika kuathirika na ugonjwa huo, wapatiwe dawa za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Aidha, Rais amewapongeza wadau wa ndani na nje ya nchi wanaoshirikiana na Serikali katika kupambana na janga la UKIMWI na kuwaomba wadau hawa wa maendeleo kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
30 Novemba, 2015
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment