MICHEZO:GUUS HIDDINK AANZA NA KAULI HII CHELSEA

Nkupamah media

LONDON,England

Meneja mpya wa klabu ya Chelsea Guus Hiddink, amekitaka Kikosi chake kuwa makini na kuzingatia uwepo wao katika Timu hiyo.
Hiddink aliteuliwa Wiki iliyopita kumbadili Jose Mourinho alietimuliwa na kupewa wadhifa huu hadi mwishoni
mwa Msimu huu.
Chelsea ambao ni Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England hadi sasa wapo Nafasi ya 15 baada ya kucheza Mechi 17 .
amesema kimahesabu chelsea inawza kumaliza katika nafasi ya nne Msimu huu ili icheze UEFA Champion Ligi Msimu ujao lakini ni kazi ngumu.
Hii ni mara ya pili kwa Hiddink kutua Chelsea mara ya kwanza ilikuwa Msimu wa 2008/09 alipotimuliwa Luiz Felipe Scolari na yeye kushika wadhifa wa Umeneja kwa Miezi Mitatu ya mwisho akiwasaidia Chelsea kutwaa FA CUP, kufika Nusu Fainali ya UEFA Champion Ligi na kumaliza Nafasi ya tatu kwenye Ligi wakiwa na Pointi saba nyuma ya Manchester United.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment