MANCHESTER,England
Meneja
wa Manchester United Louis van Gaal ambaye kwa sasa yuko katika hali
mbaya ndani ya klabu hiyo kutokana na matokeo mabovu ya timu hiyo
amezungumza kwa
ukali dhidi ya waandishi wa habari kupitia Mahojiano na
Wanahabari hao kuelekea mchezo wa Jumamosi na Timu ya Stoke City.
Kupitia
mahojino hayo Van Gaal alisema najua mtaandika yote hayo,na kwa Sasa
hatupo kwenye nafasi nzuri lakini kumbukeni Wiki nne zilizopita tulikuwa
Namba moja kwenye Ligi na baada ya Wiki nne tunaweza kuwa wa Kwanza
tena.
Mwisho
Vaan Gaal aliwaambia Waandishi katika mkutano huo kuwa Nawatakia
Krismasi njema na Mwaka Mpya mwema , na Furahieni Mvinyo na Mikate
pamoja na Nyama ya Kusaga.


0 comments :
Post a Comment