Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa
Singida, Dk. Parseko Kone alipomtembelea na kufanya mazungumzo ofisini
kwake jana mjini Singida.
Na Modewjiblog team, Singida
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Dkt. Parseko Kone ofisini kwake kwa ajili ya
kubadilishana uzoefu wa
utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mkoani humo.
Mratibu huyo yupo Mkoani hapa kwa siku mbili kukagua miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Katika
siku yake ya kwanza atatembelea mradi wa afya ambao unashughulikia watu
wanaoishi na VVU katika kijiji cha Puma wilaya ya Ikungi. Pia
atatembelea kikundi cha ufugaji nyuki kinachojihusisha na uzalishaji wa
asali na utengenezaji wa mishumaa.
Aidha akiwa kijiji cha Puma atatembelea kambi waliokolazwa watu wenye ugonjwa wa Kipindupindu.
Katika
ukaguzi wa miradi hiyo Mratibu huyo atapata nafasi ya kuzungumza na
walengwa wa miradi hiyo ili kupata mafanikio na changamoto
zilizojitokeza.
Katika
siku yake ya pili na ya mwisho mkoani Singida Bw. Alvaro Rodriguez
atatembelea mradi mkubwa wa ufugaji nyuki kisasa unaofadhiliwa na
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP).
Baada ya hapo atatembelea ujenzi wa hospitali ya rufaa inayoendelea kujengwa kijiji cha Mandewa nje kidogo ya mji wa Singida.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone alitoa Shukrani
kwa Umoja wa Mataifa kwa misaada yake ya kuisaidia serikali katika
kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Hata hivyo ameomba Mashirika hayo yaendelea kusaidia katika Nyanja za upatikanaji wa ajira kwa vijana na masoko kwa wakulima.
Mratibu
huyo baada ya kumaliza ziara yake mkoani Singida ataelekea mkoa wa
Tabora ambapo ataanza ziara yake tarehe 3 mwezi Desemba na baada ya
kumaliza mkoa wa Tabora atelekea mkoani Kigoma tarehe 4 hadi 6 nwezi
Desemba.
Singida
ni kati ya mikoa itakayounufaika na mpango mpya wa malengo ya maendeleo
endelevu (Sustainable Development Goals-SDGs) unaotarajiwa kuanza
kutekelezwa 2016-2030.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone akisalimiana na Mtaalam wa
Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu
(kulia) aliyeambatana na Bw. Rodriguez. Aliyeketi ni Katibu Tawala wa
mkoa wa Singida, Festo Kang’ombe.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (wa kwanza kulia) akiwa kwenye
mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
aliyeambatana na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Maulidah Hassan (wa tatu kushoto) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu katika ziara ya
kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mkoani
humo. Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida, Mdala
Fedes. wengine pichani ni Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo
Kang’ombe (wa kwanza kulia).
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone akisoma baadhi ya mambo yaliyomo
kwenye kitabu cha ‘Mwongozo wa wadau wa kilimo na mifugo’
kilichoandaliwa na ofisini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
(hayupo pichani). Kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Festo
Kang’ombe.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Dk. Parseko Kone.
……AKIWA NJIANI KUELEKEA MKOANI SINGIDA……
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa ameambatana na Ofisa kutoka
Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kulia) mara baada ya
kusimamisha gari maeneo ya Babati mjini.
Neema
Mikaeli (22)akihamaki kuona watu waliokuwa wakimsogelea (hawapo
pichani) katika eneo alilokuwa akifua nguo kwenye dimbwi la maji machafu
ya mvua kama yanavyoonekana pichani.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akiwa njiani kuelekea mkoani Singida
alishtushwa kuona mkazi mmoja wa Babati mjini Neema Mikaeli (22) akifua
nguo kwenye dimbwi la maji machafu ya mvua na kusimama na kuzungumza nae
ambapo aligundua kuna tatizo la maji safi na salama kwa wakazi wa eneo
hilo pamoja na ukataji miti ambao unapelekea kuharibu mazingira.
Katika
mazungumzo ya Neema alisema kuwa kuna mabomba ya maji yaliyowekwa zaidi
ya miaka 3 sasa lakini hayatoi maji na hivyo kupelekea wao kutembelea
umbali mrefu ambao kuna mto na wanatumia maji ya mto huo kupikia na
kunywa.
Akiongea
na Mikaela alimuhakikishia kwamba Umoja wa Mataifa utazidi kufanya kazi
ka ukaribu na serikali ya Tanzania sambamba na kukabiliana na
changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
Haya
ndio maji ambayo hata sabuni ya unga haikolei yaliyokutwa yakitumiwa na
Neema Mikaeli (22) (hayupo pichani) kufulia nguo zake.
Neema Mikaeli (22) akiwa kwenye eneo la dimbi la maji ya mvua akiendelea kufanya usafi wa nguo zake.
0 comments :
Post a Comment