Jeshi la polisi mkoani hapa
limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya mfanyakazi wa shirika la
hifadhi za taifa,na mkuu wa Taarifa Fiche wa shirika hilo Emily Kisamo
aliyeuwawa mwishoni mwa wiki katika eneo la Kikwakwaru Kata ya Themi
jijini Arusha.
Akizungumza na vyombo vya habari
ofisini kwa kwake jijini hapa Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa
Liberatus Sabas alisema jeshi hilo limefanikwa kumkamata mtu anayeitwa
Ismail Swalehe Sang’wa 20 mtunza bustani mkazi wa Sepuka Wilayani Ikungi
mkoani Singida.
Alisema kuwa siku ya tukio
mtuhumiwa alimvizia marehemu akinywa uji Sebuleni na kumkata shingoni
kwa kutumia kitu chenye ncha kali,baada ya kukamatwa mtuhumiwa aliweza
kueleza jinsi alivyotekeleza mauaji hayo huku akieleza pia sababu za
kufanya hivyo ni tama ya pesa alizokuwa nazo marehemu hapo kiasi cha
tsh. Million 5.
Kamnda Sabas aliendelea kusema
kuwa baada ya kufanya mauaji hayo mtuhumiwa alikiri kwamba alianza usafi
wa ndani ya nyumba kwa kupiga deki na kasha kulisafisha gari kwa nje na
kuliendesha mpaka eneo alipolitelekeza gari la marehemu Kisamo.
Mara baada ya upekuzi polisi
waligundua vitu kadhaa kwenye gari hilo vikiwemo fedha taslimu kiasi cha
Tsh.Milion 4.29,4000,simu za mkononi tatu. Aina ya Samsung,na vocha
aina ya Vodacom za 5000 zenye thamani ya 70000 vyote hivyo vilifukiwa
kwenye banda la kuku.
Pia polisi waligundua panga moja
lililokuwa na damu ambalo lilikutwa stoo na vitu vingine kama taulo
kubwa nne,kitambaa cha mezani,suruali moja ya mtuhumiwa ambazo
zilifichwa kwenye migomba karibu na mabanda ya kuku na zilikuwa na damu
ambapo ndizo zilitumika na myuhumiwa kupigia deki ndani baada ya kumuua
marehemu.
Kamanda alisema kuwa kufuatia
tukio hilo jeshi la polisi mkoani hapa linaendelea na upelelezi na pindi
utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili.
Wakati huo huo jeshi la polisi
liemsema kuwa limejipanga kuhakikisha wakazi wa mkoa huo wanasherehekea
sikukuu zote Maulid na Krismas kwa amani na utulivu na kuwataka wakazi
wote kuhakikisha hawafanyi vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa
amani.
Kamanda wa jeshi Hilo mkoani
hapa Liberatus Sabas pia akawatakiwa wakazi hao sikukuu njema na yenye
Baraka itakayoendana na kukukaribisha mwaka bila ya kuvunja sheria za
nchi na kufanya matukio ya fujo na kushrehekea kwa amani sikukuu hiyo
0 comments :
Post a Comment