Msanii mwenye kipawa cha kuimba nchini
Tanzania Ali Kiba anatarajia kusherekea mwaka mmoja tangu aliporudi
kwenye ramani ya muziki baada ya kupotea kwa muda wa miaka mitatu,
Alikiba anataraji kufanya
onyesho la kufunga mwaka siku ya Boxing Day
Disemba 26 kwa kutumbuiza nyimbo zake kali huku akiwa na band yake.
Katika kuelekea sikukuu watu maarufu
hujitahidi kuonesha furaha zao kusherekea na watu mbalimbali wasio kuwa
na uwezo, kwa upande wake Alikiba ameamua kutoa asilimia kumi ya mapato
kwenye onyesho lake kusaidia watoto yatima kupitia Foundation ya
mtangazaji Diva the Bawse iitwayo Diva Foundation ambapo fedha zote
zitapelekwa kwenye mfuko wa Diva Giving for Charity.


0 comments :
Post a Comment