Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasili katika Viwanja vya Karim Jee jijini Dar es Salaam katika sherehe za Maulid.
Picha na Raymond Mushumbusi Maelezo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akifurahi jambo, alipokuwa akishiriki katika sherehe za Maulid
(Kushoto)
Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakari Bin Zuberi Bin Ali na kulia ni
Rais Msataafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia sherehe za Maulid zililofanyika katika viwanja vya Karim Jee.
Baadhi ya waumini
wa dini ya Kislamu wakifatilia hotuba na mawaidha mbalimbali wakati wa
sherehe za Maulid zililofanyika katika viwanja vya Karim jee Jijini Dar
es salaam.
Msanii wa sanaa
ya maigizo Tanzania Ahmed Olutu maarufu kama Mzee Chilo akifatilia
sherehe za Maulid zililofanyika katika viwanja vya Karim jee Jijini Dar
es salaam.
Waziri Mkuu
Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akijadili jambo na baadhi ya wawakilishi
wananchi mmbalimbali wakati wa sherehe za Maulid zililofanyika katika
viwanja vya Karim jee Jijini Dar es salaam.
vijana wa kislamu
wakicheza kaswida katika kusherekea Sikukuu ya Maulid wakati wa Baraza
la Maulid zililofanyika katika viwanja vya Karim jee Jijini Dar es
salaam.
……………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Watanzania wameaswa kuiendeleza amani na
utulivu iliyopo kwa sasa nchini na kutoiacha ikapotea kwani ndio nguzo
muhimu kwa watanzania na mstakabali wa maendeleo ya nchi yetu kiujumla.
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu Mhe
Kassimu Majaliwa alipokuwa akihutubi Baraza la Maulid lililofanyika
katika viwanja vya karim Jee Jijini Dar es salaam na kuwaasa waislamu
wote nchini na watanzania kiujumla kudumisha upendo amani na mshikamano
uliopo.
Waziri mkuu Kassimu Majalimu ameongeza kuwa
serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za kidini katika kulenda
maendeleo na kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo Elimu na Afya.
Pia ameitaka jamii ya kislamu na watanzania
wote kuzingatia maadili mema na kuwafundisha watoto maadili mazuri ili
kupunguza wimbi la uvunjivu wa maadili nchini ambao unasababisha vijana
wengi kupotea katika madawa ya kulevya na kupata mimba za utotoni.
“Sisi kama Serikali ya Awamu ya Tano tuko
makini sana na tunatoa shukrani kwa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania
(BAKWATA) kwa kushirikiana na sisi katika maswala mbalimbali ya
kimaendeleo na sisi tutashirikiana nanyi bega kwa bega” Alisema Waziri
Mkuu Majaliwa.
Naye Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakari
Bin Zuberi Bin Ali amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano na kumpongeza pia kwa
kumteuwa Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa na kuteuwa mawaziri makini katika
kuiletea maendeleo nchi yetu.
Waislamu wote Duniani leo wanaikumbuka siku
ya kuzaliwa Mtume wao Mohamed SAW na kwa Tanzania maadhimisho hayo
yamefanyika kitaifa katika viwanja vya Karim Jee Jijini dare s salaam
nakuhudhuriwa na viongozi wa chini dini, na mabalozi mabalimbali
waislamu na wanachi wa dini zote.
0 comments :
Post a Comment