Nkupamah media
Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inakanusha taarifa zilizoandikwa
katika gazeti la Mwananchi la tarehe 24.12.2015 yenye kichwa cha habari
“JPM kutolipa makocha Stars”.
Serikali
kupitia Wizara inayohusika na michezo haijatoa tamko la kutowalipa
makocha wanaofundisha timu ya Taifa Stars kama ilivyoripotiwa na gazeti
hilo.
Suala
la malipo ya makocha wa Taifa Stars linashughulikiwa kwa mujibu wa
sheria na taratibu za Serikali, pindi maamuzi yatapofikiwa, serikali
itatoa maelekezo kama itaendelea kuwalipa au la.
Serikali
ya Awamu ya Tano inathamini michezo yote ikiwemo mpira na miguu , kwa
hiyo itaendelea kushirikiana na Vyama vya vyote vya michezo na wadau
wote wa michezo kwa ujumla katika kuhakikisha kuwa michezo inaimarika na
kuwa chanzo cha ajira kwa vijana nchini.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)
24 DESEMBA, 2015
0 comments :
Post a Comment