Nkupamah media
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi waendelee kulinda
amani ya nchi huku akikemea uvaaji wa nguo fupi na kuwasihi Watanzania
kujenga tabia ya kuvaa mavazi yenye kumpendeza Mungu.
Pia,
amekemea matumizi ya dawa za kulevya na mimba za utotoni akisema ni
mambo ambayo yanaepukika kwa mtu yeyote aliyelelewa katika misingi ya
kidini.
Waziri Majaliwa alisema hayo jana alipokuwa akihutubia Baraza la Maulid lililofanyika Karimjee jijini Dar es Salaam.
Alisema
mambo yote hayo yanawezekana kama watu watamkimbilia Mungu huku
akiwaomba viongozi wa dini kuwausia waumini wao kuvaa mavazi ambayo
yanampendeza Mungu.
“Mtoto akilelewa kwenye mazingira ya dini itakuwa ngumu kuvaa mavazi ambayo hayampendezi Mungu,” alisema.
Amesema
Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini zile ambazo ziko
kisheria huku akizitaka ziendelee kuisaidia Serikali kwa kujenga shule
na hospitali na kutoa huduma nyingine za kijamii.
Waziri Majaliwa
alitumia fursa hiyo kuwapongeza Watanzania kwa kuwa watulivu katika
kipindi chote cha uchaguzi hadi ulipofanyika Oktoba 25.
Akizungumza
katika baraza hilo, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti, Abubakari Zuberi
aliwaasa waumini wa Kiislamu kufanya mambo yote yanayompendeza Mwenyezi
Mungu.
Aliwashukuru Waislamu wote nchini kwa kushirikiana na wananchi wenzao ambao siyo wa dini hiyo katika kudumisha amani.
0 comments :
Post a Comment