@nkupamah blog
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando
Na Magreth Kinabo- MAELEZO
Serikali
imewaagiza maafisa wa afya nchini kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo
bora ikiwa ni hatua ya kuhakikisha jamii inaepekana na magonjwa
yanayotokana na uchafu mazingira , sambamba na suala la usafi wa
mazingira kuwa endelevu kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha Serikali imepiga marufuku ulaji wa
matunda yaliyomenywa barabarani.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Dkt. Donan Mmbando, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
Katibu
Mkuu huyo ambaye alikuwa ameambatana na baadhi ya viongozi kutoka Ofisi
ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu, wakiwemo wa wizara yake kwa
ajili ya kuzungumzia mambo matatu ambayo ni suala la usafi wa mazingira
katika kuadhimisha siku ya Uhuru ,Desemba 9, mwaka 2015, ugonjwa wa
kipindupindu na polio.
“Wakuu wa
mikoa na wilaya wanatakiwa kutekeleza agizo hili kwa kujiwekea
utaratibu wa kufanya usafi maeneo yao,” alisema Dkt. Mmbando.
Dkt.
Mmbando alisema ikumbukwe kuwa ugonjwa wa kipindupindu pamoja na
magonjwa mengine yanayohusiana na uchafu huenea kwa kasi kutokana na
hali duni ya usafi katika maeneo tunayoishi. Hivyo takwimu zinaonesha
kuwa kati ya taka ngumu zinazozalishwa ni 50% tu huzolewa na kupelekwa
dampo. Kiasi cha taka kinachobaki huzagaa katika maeneo mbalimbali
hususani kando kando ya barabara, katika maeneo ya kukusanyia taka
(Collection points), chini ya madaraja na katika maeneo ya wazi hali
inasayobabisha miji yetu kuonekana michafu.
“Hali
kadhalika, takwimu zinaonesha kuwa ni kaya zipatazo 34% ndizo zina vyoo
bora na asilimia 12% hazina vyoo kabisa. Hali hii inahatarisha afya ya
jamii na kusababisha kuenea kwa urahisi kwa magonjwa ya kuambukiza. Kwa
mijini na miji midogo, mifereji ya maji taka na ile ya mvua ni michafu
na mingi imeziba, hivyo hutiririsha maji ovyo na kuhatarisha afya ya
jamii,” alisema .
Aliwataka
watendaji hao, kusimimia suala hilo kwa kuzingatia sheria za afya
zilizopo, huku akizitaka halimashauri na mamlaka kuweka sheria ndogo
ndogo ambazo hazileti unyanyasaji kwa wananchi. Katika kutekeleza kwa
vitendo agizo la Mhe. Rais .
Kubainisha
maeneo yote ya umma ambako shughuli za usafi wa mazingira zitafanyika
siku hiyo,kuhamasisha jamii kwa njia mbalimbali kujitokeza kwa wingi
kushiriki shughuli za usafi katika maeneo yao na sehemu za kazi au
biashara, vyombo vya usafiri wa abiria na vituo vya wasafiri ili
vifanyiwe usafi wa kuridhisha,kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo
sekta binafsi, vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi za elimu, n.k. ili
kufanikisha zoezi zima la ukusanyaji, usafirishaji na utupaji salama wa
taka (madampo) kutoka katika maeneo ya kaya, umma na taasisi kwa siku
hiyo.
Aliongeza
kwamba wanapaswa kuhusisha au kushirikisha vyombo vya habari vya
kitaifa na kijamii katika kuhamasisha jamii kushiriki zoezi la
usafi,kupanga ratiba na wajumbe wa kusimamia kazi hiyo katika
halmashauri kwa tarehe 9,Desemba,2015 kwenye maeneo ya kaya na ya umma
na kupanga ratiba endelevu baada ya hapo,kuwasilisha taarifa za
utekelezaji wa kazi hizi kwa mfumo na muda ulioinishwa na Wizara.
Pia kwa
kushirikiana na wadau, halmashauri zina wajibu wa kuandaa vyombo vya
usafirishaji taka ngumu na maji taka kutoka maeneo ya uzalishaji hadi
maeneo yaliyoainishwa kutupwa bila kuathiri mazingira.
Kwa
upande wa wananchi aliwataka wafanye yafuatayo ili kupambana na kuenea
kwa ugonjwa wa kipindupindu kila mmoja Kuchemsha maji ya kunywa au
kutibu kwa dawa maalumu (waterguard)Kuepuka kula chakula kilichopoa au
kuandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salamaKunawa mikono kwa
sabuni na maji safi na salama,kabla ya kula,baada ya kutoka chooni.
Mambo
mengine ni baada ya kumnawisha mtoto aliyejisaidia,baada ya kumhudumia
mgonjwa,kuosha matunda kwa maji safi kabla ya kula,Kukomesha
utiririshaji wa maji kutoka chooni ,Kutoa taarifa katika kituo cha
kutolea huduma za afya endapo utapatwa na ugonjwa wa kuharisha au
kutapika,kutoa taarifa kwenye ofisi za serikali endapo mtu au kikundi
cha watu kitafanya shughuli zenye kuashiria uchafuzi wowote wa
mazingira.
Aliongeza
kwamba Serikali itaendeleza juhudi za kuwezesha wananchi kupata maji
safi na salama. Napenda kusisitiza kwa wananchi wote, tuwe makini
kutumia maji yanayotoka katika vyanzo visivyo salama. Hii ni muhimu
kwani, kwa sehemu kubwa, ugonjwa huu huenezwa kupitia maji yasiyo
salama.
Tangu
kutokea kwa ugonjwa huu kwa mara ya kwanza tarehe 15 Agosti, 2015 katika
mkoa wa Dar es Salaam ugonjwa huu umeendelea kusambaa kwa kasi. Hadi
tarehe 2/12/2015 Mikoa mingine 20 ya Morogoro, Iringa, Pwani,
Kilimanjaro, Kigoma, Dodoma, Geita, Mwanza, Arusha, Mara, Shinyanga,
Tabora, Singida, Tanga, Lindi, Rukwa, Manyara, Kagera, Katavi na Mbeya
imeshaathiriwa.
Takwimu
zinaonesha kuwa hadi tarehe 2 Desemba, 2015 jumla ya watu 9,906 walipata
ugonjwa huu na kati yao jumla ya watu 149 wameshafariki dunia kutokana
na ugonjwa huu. Aidha, wagonjwa wengine wamepata matibabu na kuruhusiwa
kurudi nyumbani ambapo hadi tarehe 2 Desemba, 2015 jumla ya wagonjwa 128
waliendelea kupatiwa matibabu katika vituo vya kutolea huduma.(P.T
0 comments :
Post a Comment