@nkupamah blog
Dk. Nalin
Nag Mshauri Mwandamizi wa madawa, aleji, upungufu wa kinga pamoja na
magonjwa ya kuambukiza kutoka hospitali za Apollo; New Delhi.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZDPY0ej4WrrE57f8TmMCAjUVOmpijrGPFp6vrxAABQcdT7vPNEY6S5IoplgScq11M9qNh0rtVsWKySt78WidBw8XKLNTNw6mC92QlIXCkO4FnX3ik_ZQSjBMKOoTmRZ-DprE6gaGuPlDB/s640/A+2.png)
Na Mwandishi wetu,
Siku ya
UKIMWI duniani inaadhimishwa tarehe mosi desemba kila mwaka, kutoa fursa
kwa jamii kuungana ulimwenguni kupiga vita gonjwa la UKIMWI, kuwapa
moyo wale wote wanaoishi na virusi vya ukimwi na
kuwakumbuka wote
waliokufa kwa ugonjwa huu. Siku ya ukimwi duniani iliadhimishwa kwa mara
ya kwanza mwaka 1988.
Zaidi ya
miaka 30 toka ukimwi ulipoanza kusambaa nchini Tanzania, msisitizo
umewekwa kwenye maendeleo ya mikakati na mbinu zaidi za kupunguza
maambukizi na kuongeza huduma za matibabu. Kwa mwaka 2011, inakadiriwa
watanzania milioni 1.6 walikuwa wanaaishi na virusi vya UKIMWI na
miongoni mwao, milioni 1.3 ni wenye umri zaidi ya miaka 15, hiyo ni kwa
mujibu wa takwimu za mwaka 2012 kutoka shirika la umoja wa mataifa la
kupambana na UKIMWI (UNAIDS). Licha maambukizi ya UKIMWI kwa Tanzania
bara yamepungua kutoka asilimia 7.0 hadi 5.3 katika kipindi cha mwaka
2003/2004 mpaka 2011/2012 miongoni mwao wakiwa watu wenye umri wa miaka
15-49 na kutoka asiimia 6.3 mpaka 3.9 ambao ni wanaume katika kundi
hilo, na hakuna takwimu nzuri za kuonyesha kupungua kwa maabukizi kwa
upande wa wanawake.(P.T)
Kwa
mujibu wa TACAIDS taarifa za mwaka 2013, kwa tanzania bara maambukizi
kimikoa yanatofautiana kutoka asilimia 1.5 kwa mkoa wa Manyara hadi
asilimia 14.8 kwa mkoa wa Njombe.
“Kufikia
sifuri tatu” ndio kauli mbiu iliyochaguliwa na kampeni ya siku ya
ukimwi duniani kuadhamisha ya siku ya UKIMWI duniani kwa mwaka huu.
Kwetu tanzania kupitia TACAIDS tunahamasisha “kufikia sifuri tatu”
tukimaanisha “sifuri katika maambukizi mapya ya UKIMWI”, sifuri katika
kuwanyanyapaa na kuwanyanyasa waathirika, na sifuri katika vifo
vinavyohusisha UKIMWI”. Maudhui hayo yalipitishwa tokea mwaka 2011
yatumike mpaka 2015, yakitafsiri yale malengo ya UNAIDS ya kufikisha
kiwango cha “kufikia sifuri katika maambukizi mapya ya UKIMWI”, na
sifuri katika vifo vinavyohusisha UKIMWI”. Maamuzi ya kuchagua “kufikia
sifuri tatu” yalifikiwa baada ya mahojiano ya kina na watu wanaoishi na
virusi vya UKIMWI, wanaharakati wa afya na taasisi ya kijamii.
Katika
kuweka msisitizo katika maudhui ya mwaka huu, “kufikia sifuri tatu”, Dk.
Nalin Nag mshauri mwandamizi wa madawa, aleji na upungufu wa kinga
pamoja na magonjwa ya kuambukiza kutoka hospitali za Apollo; New Delhi
anawaasa watanzania kuepuka maambukizi mapya ya UKIMWI, kuepuka
kunyanyapa waathirika wa UKIMWI katika familia na jamii zetu na
ikiwezekana kufuta kabisa vifo visababishwavyo na UKIMWI.
”UKIMWI
ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wetu na tunaweza kupambana nacho kwa
urahisi zaidi ya mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa kwa kushtukizwa-
“kufikia sifuri” katika maambukizi ya UKIMWI inawezekana kabisa kama
wote tukidhamiria. Alisisitiza Dk. Nalin Nag
Mtazamo
chanya katika maisha, ushirikiano kutoka katika familia na marafiki,
malalamishi ya ukandamizwaji kutoka kwenye jamii kwa wingi wa watu
wanaoishi na virusi vya UKIMWI ni tatizo la muda tu. Sheria kali
zinahitajika kulinda na kutunza utu wa wahanga wa janga hili. Aliongeza
Dk. Nalin Nag.
Dk. Nalin
Nag anasisitiza kuwa wagonjwa UKIMWI wafanye vipimo vyote vya afya zao
mara kwa mara, vipimo vya damu maabara, ufanisi wa ini, figo, kifua na
tatizo la hepatitis B. magonjwa nyemelezi kama kifua kikuu, pneumonia na
mengineyo yanatakiwa kudhibitiwa muda wote kabla ya kuanza kutumia dawa
za ARV.
“mlo
sahihi, uongezaji wa kinga, mitindo ya maisha, na namna ya kupambana na
msongo wa mawazo ni vitu vinavyojumuisha mlolongo wa kuboresha maisha
bora kwa waathirika ambao kwa sasa wanatarajia kuongeza muda wa maisha
yao kwa matumizi sahihi ya ARV. Alisema.
Dk. Nalin
Nag anaelimisha jamii kuhusu umuhimu wa matumii ya dawa za ARV kwa
waathirika wote wa UKIMWI. Hii imebadilisha kabisa makali ya ugonjwa na
kuongeza ujasiri katika kutokomeza maambukizi mapya. Dawa tofauti za ARV
zinapatikana na zinatumika zikiwa na kinga za aina 4 tofauti kwa ajili
ya kudhibiti nguvu za virusi na kupunguza makali ya ugonjwa.
“katika
mazingira mengine huwa virusi havionekani kwenye damu hadi mwishoni mwa
miezi sita hadi mwaka” aliongeza Dk. Nalin Nag kutoka Hospitali za
Apollo Indraprastha.
Katika
kitengo cha afya ugonjwa wa UKIMWI unabaki kuwa changamoto kubwa
ulimwenguni, hasa kwa wananchi wenye kipato cha chini au cha kati. Na
matokeo ya hivi karibuni kuhusu upatikanaji rahisi wa ARV, kumefanya
wagonjwa wa UKIMWI kuweza kuishi maish marefu zaidi yenye afya bora. Kwa
kuongezea, imedhibitishwa kuwa ARV inaepusha maambukizi endelevu ya
UKIMWI.
UKIMWI
umeendelea kuenea ulimwenguni, kwa mujibu wa taarifa za sasa za shirika
la umoja wa mataifa la kupambana na UKIMWI (UNAIDS) takwimu za mwaka
2012, inakadiriwa watu milioni 34 wanaishi na virusi vya UKIMWI zaidi ya
jinsi ilivyokuwa awali nah ii pia ni kutokana na matumizi ya dawa za
ARV. Nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara zimebaki kuwa nchi
zilizoathirika zaidi na janga hili la UKIMWI. Mwaka 2011, ilikadiriwa
kuwepo kwa maambukizi mapya milioni 1.8 kwa nchi hizo; asilimia 69 ya
watu wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI wanapatikana katika nchi
zilizopo chini ya jangwa la Sahara barani Afrika (UNAIDS, 2012).
Kuhusu Hospitali za Apollo
Hospitali
ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho
imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta
huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma
bora na mafanikio katika elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya
kibinadamu".Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo
imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya
kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi
makubwa katika sekta ya afya nchini india.
Katika
safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka
nchi 120.Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710.Imefanya
upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000
za mishipa myembamba.Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha
idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na
zaidi.Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india,
zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji
unaotumia mashine za kiroboti.
0 comments :
Post a Comment