TIMU ya soka ya Jitegemee Fc imewezwa kuutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Kawambwa Cup baada ya kuitandika timu ya Buma Fc kwa mabao 2-0 zote za Wilayani bagamoyo katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Mwanakalenga mjini hapa.
Katika mchezo huo ambao
ulihidhuliwa na umati mkubwa na mashabiki kutoka maeneo mbali mbali ya
Bagamoyo na Jijini Dar es Salaam uliweza kuwavutia wengi kutokana na
kila timu kuonyesha kandanda la kufundishika katika kipindi chote cha
dakika 90 za mchezo huo.
Wachezaji wa timu ya Jitegemee Fc walianza mpira kwa kasi kwa kupeana pasi za kiufundi nakulisakama lango la wapinzani wao ambapo waliweza kuandika bao la kwanza kunako katika dakika ya 10 lililofungwa na mshambuiaji wao wa kutumainiwa Frank Raiko.
Kuingia kwa bao hilo
kulionekana kuwachangannya wachezaji wa timu ya Buma fc na kujaribu
kuelekeza mashambulizi yao ya kushitukiza lakini kutokana na safu ya
ulinzi wa timu ya jitegemee kuwa imara waliweza kuzuia mashambulizi
hayo.
Dakika ya 30 mchezji Yahaya
Ramadhani aliweza kuwainua mashabiki wa timu yake ya Jitegemee baada ya
kupachika bao la pili na kumwacha minda mlango wao Mbwana Matola akiwa
ameduwaa na mpira huo kuzama nyavuni.
Hadi kipenga cha dakika 90 kinapulizwa timu ya Jitegemee Fc iliweza kuibuka kidedea kwa ushindi huo wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao na kutawazwa rasmi kuwa mabingwa katika mashindano hayo ya Kawambwa Cup kwa mwaka 2015.
Katika fainali za mchezo huo
ambao ulihudhuriwa na katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu
Tanzania i (TFF)Selestine Mwesigwa ambapo aliikabidhi timu ya Jitegemee
zawadi ya kombe,seti ya jezi ,mipira miwili ,pikipiki na medali ya
dhahabu .
Mshindi wa pili alikuwa ni Buma
Mjini waliopatiwa seti ya jezi na mipira,na mshindi wa tatu timu ya
Mwambao ilikabidhiwa seti ya jezi na mipira na timu yenye nidhamu
pamoja na kipa bora walipatiwa zawadi ya ngao .
Katibu Mwesigwa alimpongeza mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dr Shukuru Kawambwa kwa kuandaa mashindano hayo kwa vijana kwa miaka kumi mfululizo ambayo lengo lake kubwa alisema ni kukuza vipaji na kuwataka wabunge wengine nchini waweze kuiga mfano huo kama huo.
Katibu Mwesigwa alimpongeza mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dr Shukuru Kawambwa kwa kuandaa mashindano hayo kwa vijana kwa miaka kumi mfululizo ambayo lengo lake kubwa alisema ni kukuza vipaji na kuwataka wabunge wengine nchini waweze kuiga mfano huo kama huo.
Kwa upande wake mwandaaji wa
michuano hiyo Dr. Kawambwa aliwashukuru wadau wote walioshirikiana nae
kufanikisha mashindano hayo na kusema kuwa mashindano hayo yamedumu kwa
miaka 10 mfululizo ambapo ameahidi kuyaboresha na kuyaendeleza katika
kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.
Kivumbi cha mashindano hayo ya
Kawambwa Cup yalianza kutimua vumbi lake rasmi Novemba 24 ,ambapo jumla
ya timu 73 kutoka kata saba za jimbo la Bagamoyo ziliweza kushiriki.
0 comments :
Post a Comment