KATIKA MSAKO WA KWANZA,
MTU MMOJA MKAZI WA NJISI WILAYA YA KYELA AITWAYE ANORD JASON [36]
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA
MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO
ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE
20.12.2015 MAJIRA YA SAA 17:30 JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA LUBELE, KATA YA NJISI, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA
KYELA, MKOA WA MBEYA.
KATIKA MSAKO WA PILI,
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA STAMICO WILAYA YA CHUNYA AITWAYE JOSEPHINE
MWASHILINDI [37] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA
POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5 ½.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
20.12.2015 MAJIRA YA SAA 15:20 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA STAMICO,
KIJIJI NA KATA YA MKOLA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA.
KATIKA MSAKO WA TATU, JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KAMFICHENI
WILAYA YA CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRANK WILSON [30] AKIWA NA
BHANGI UZITO WA KILOGRAM MBILI [02].
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
20.12.2015 MAJIRA YA SAA 18:30 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
KAMFICHENI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA NA POMBE MOSHI [GONGO] KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments :
Post a Comment