Waziri
Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) akipata maelekezo toka kwa
Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China
Bw. GAO Wei (kulia) wakati Waziri Mkuu akifungua kituo cha Utamaduni wa
China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel.Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
Mshauri
wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw.
GAO Wei akitoa ufafanuzi wa picha za matukio mbalimbali kwa Waziri Mkuu
mstaafu Mizengo Pinda (katikati) mara baada ya Waziri Mkuu Mstaafu
kufungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo
jijini Dar es Salaam.
Kundi
la Muziki la Zinijncheng kutoka chuo Kikuu cha Sanaa ya Muziki cha
China kikitoa burudani kwa mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda
(hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi
wa kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania.
Baadhi
ya wanafunzi wa Kitanzania wanaojifunza lugha ya Kichina katika kituo
cha Utamaduni wa China nchini Tanzania wakiimba nyimbo kwa lugha ya
Kichina mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo
pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo
hicho.
Waziri
Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (kushoto) akifungua kituo cha utamaduni wa
China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni toka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko.
0 comments :
Post a Comment