Balozi wa Jamhuri ya Watu wa
China nchini Tanzania, Lu Youqing , akisaini kitabu cha wageni mara
baadaya kuwasili katika Ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kulia), ofisini kwake alipowasili Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi kwa ziara fupi.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa
China hapa nchini, Lu Youqin akizungumza katika kikao na Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi. Mhe. Charles Kitwanga (wa pili upande wa kushoto).
Katika kikao hicho kilichofanyika Wizara hapo, viongozi hawa walijadili
masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Serikali ya China na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhe. Charles Kitwanga (wa kwanza upande wa kulia), akimsikiliza Balozi
wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lu Youqing (wapili upande
wa kushoto) wakati wa mazungumzo yaliyohusu masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati Serikali ya China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mazungumzo hayo yalifanyika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar
es Salaam..
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (wa nne kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na
ujumbe kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania, ulioongozwa na Balozi
Lu Youqing (watatu kutoka kulia). Ujumbe huo ulitembelea Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi kujadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
(PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)


0 comments :
Post a Comment