Gambia: Wafanyakazi wa kike wajifunike nywele


Jammeh


 Jammeh ameongoza Gambia kwa miaka 21
Serikali ya Gambia imepiga marufuku wafanyakazi wa kike kufika kazini wakiwa hawajajifunika nywele.
Kupitia barua iliyofichuliwa na magazeti ya kibinafsi nchini humo, serikali ya nchi hiyo inasema
wanawake lazima "wafunge nywele zao na kitambaa'' barua hiyo haikutoa sababu yoyote ya kupiga marufuku.
Mwezi uliopita, Rais wa Gambia Yahya Jammeh alitangaza nchi hiyo yenye Waislamu wengi kuwa jamhuri ya Kiislamu.
Aliongezea kuwa watu wasio Waislamu hawangelazimishwa kuvalia mavazi ya Kiislamu.
Gambia ni maarufu sana kwa watalii kutoka magharibi kutokana na fukwe zake.
Mwaka 2013, Rais Jammeh aliondoa taifa hilo kutoka kwa Jumuiya ya Madola akisema muungano huo wa Uingereza na mataifa yaliyotawaliwa na Uingereza ni ukoloni mamboleo.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment