wa haki miliki za kitabu cha Mein Kampf zimekuwa zikishikiliwa na jimbo la Bavaria
Kitabu
kilichoandikwa na kiongozi wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler kitaanza
kuuzwa
tena baada ya hakimiliki za kitabu hicho kufikia kikomo.
Kitabu hicho kwa jina Mein Kampf kilipigwa marufuku baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na serikali ya Bavaria, ambayo ilimiliki haki za kitabu hicho.
Hii ina maana kwamba hakuna yeyote ambaye angeweza kuchapisha au kusambaza kitabu hicho kwa miaka 70.
Kwa mujibu wa Sheria Ujerumani, hakimiliki hudumu kwa miaka 70.
Sasa hakimiliki ya kitabu hicho imefikia kikomo na Taasisi ya Historia ya Kisasa (IfZ) mjini Munich imesema itaanza kuuza nakala za kitabu hicho wiki ijayo.
Nakala za kitabu hicho kinachoangazia sera aliyoifuata Hitler kilikuwa mwongozo wa utawala wa Nazi.
Lakini wanahistoria wanasema kitabu hicho Mein Kampf (Mapambano au Mapigano yangu) kitasaidia wasomi kufahamu yaliyotendeka wakati wa uongozi wa Nazi.
Mein Kampf kilichapishwa mara ya kwanza 1925, miaka minane kabla ya Hitler kuingia mamlakani.
Majeshi ya muungano yaliyoshinda vita dhidi ya Ujerumani 1945 yalikabidhi hakimiliki ya kitabu hicho kwa jimbo la Bavaria.


0 comments :
Post a Comment