Michuano ya Kombe la Shirikisho
(Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa tatu inatarajiwa kuendelea
Januari 12 na wikiendi ya Januari 23-27 kwa timu 32 kuchuana kuwania
kufuzu kwa
hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya
Vodacom zimeingia moja kwa moja mzunguko wa tatu ambapo sasa
zinajumuika na timu 16 zilizofuzu kutoka raundi ya pili yenye timu
kutoka ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili.
Jumamosi, Januari 12, Majimaji
itacheza dhidi ya JKT Mlale uwanja wa Majimaji mjini Songea, Januari 23
Pamba v Toto Africans uwanja wa CCM Kirumba, Ndanda FC v Mshikamano
Nagwanda Sijaona Mtara, huku Burkinafaso wakiwakaribisha Simba SC katika
uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Januari 24, Young Africans
watacheza dhidi ya Friends Rangers uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
Njombe Mji v Tanzania Prisons uwanja wa Amani Makambako, mjini
Shinyanga Stand United watachuana dhidi ya Mwadui FC.
Mechi zingine ni Kagera Sugar v
Rhino Rangers, Panone v Madini, Mtibwa Sugar v Abajalo, Lipuli/Kurugenzi
v JKT Ruvu, Ashanti United v Azam FC, Africa Sports v Coastal Union,
Geita Gold v Mgambo Shooting, Singida United v Mvuvuma na Wenda v Mbeya
City.
Timu 15 zilizofuzu hatua ya tatu
kutoka raundi ya pili ni Ashanti United, Friends Rangers, Panone, Geita
Gold, Pamba, Mvuvuma, Burkinafaso, Rhino Rangers, Madini FC, JKT Mlale,
Mshikamano FC, Njombe Mji, Wenda FC, Singida United, Abajalo huku mchezo
mmoja kati ya Lipuli dhidi ya Kurugenzi ukichezwa leo hii kusaka timu
ya kufuzu raundi ya tatu.
Bingwa wa michuano ya Kombe la
Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye
Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.


0 comments :
Post a Comment