…………………………………………………………..
Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi
imeweka zuio la kubomoa nyumba zilizopo katika wilaya ya Kinondoni hasa
zile ambazo wamiliki wameleta ombi lao mahakamani kuzuia kubomolea.
Akitoa hukumu hiyo mbele ya walalmikaji
Mwanasheria wa Serikali, mawakili wa walalmikaji na wananchi Jaji wa
Mahakama hiyo kuu ya Ardhi Mhe.Panterine Kente amesema kuwa mahakama
imezingatia maelezo toka pande zote mbili na kuangalia madhara
watakayopata wananchi kwa kutekelezwa kwa zoezi hilo.
Jaji Panterine Kente ameongeza kuwa mahama
ya Ardhi haijaweka zuio la bomoa bomoa kwa Tanzania nzima bali kwa wale
tu walioleta maombi ya shauri la zuio la kubomolewa nyumba zao na
kusisitiza kuwa Serikali itaendelea na uwekaji wa alama za x na ubomoaji
wa nyumba zilizopo sehemu hatarishi na sehemu zisizostahili.
“ Nakuagiza Wakili Abubakari Salim uniletee
majina yote leo hii na sio kesho ya waliofungua shauri la zuio la
kutobomolewa nyumba zao ili tuweze kuendelea na zoezi la ubomoaji”
Alisema Jaji Kente
Akizungumza baada ya kutolewa hukumu hiyo
Wakili wa Serikali Manchare Henche amesema wamepokea hukumu hiyo na wao
wataendelea na majukumu yao ya ubomoaji wa meneo hatarishi kama
Mahakama ilivyoeleza kuwa haijatoa zuio la bomo bomoa kwa Tanzania nzima
ila kwa wale tu walioleta shauri la zuio.
“Tunaomba walio maeneo ya mabondeni wahame
kwani zoezi hili linaendela na zoezi la uwekaji wa alama za x
litaendelea kama kawaida kwa maeneo mengine nje ya haya yaliyowekewa
zuio” Alisema Subuta.
Aidha akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kutolewa hukumu hiyo Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia
amesema kuwa uamuzi umeridhisha na pia mahakama imetenda haki kwa
wananchi wa kinondoni na wanashukuru kwa kupata nafasi ya kusikilizwa
kwa hoja zao.
Kesi hiyo namba 822ilifunguliwa na
wawakilishi nane wanaowawakilisha wanachi 674 ambao nyumba zao zilikuwa
katika mpango wa kubomolewa chini ya sheria za mipango miji.
Baada ya Mahakama kuu ya Tanzania kitengo
cha Ardhi kutoa zuio la bomoa bomoa kwa wakzi hao kesi ya msingi
itatajwa tena januari 11

0 comments :
Post a Comment