Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Sylvester Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini
jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katika ziara
hiyo, Naibu Waziri Masauni aliiagiza Idara hiyo kuchunguza Makapuni
yanayotoa ajira kwa
wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye
sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini.. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni (kulia) akiwasalimia wananchi wanaosubiri kupata
huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji,
Kurasini, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake kwa Viongozi Wakuu wa
Idara hiyo, Naibu Waziri Masauni aliiagiza Idara hiyo kuchunguza
Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa
Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Afisa Uhamiaji anayeshughulika na
uchapaji wa Hati za Kusafiria, Amir Hassan (kushoto), akitoa maelezo
ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria, kwa Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati aliyevaa tai) ambaye alifanya
ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini,
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Sylvester Ambokile. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kumaliza kikao chake na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati
alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini
Dar es Salaam leo. Wakwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Sylvester Ambokile, na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel
Mgonja. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna wa Idara ya Uhamiaji
(Utawala na Fedha), Piniel Mgonja akitoa taarifa fupi ya utendaji wa
Idara hiyo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni
(katikati) wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao
Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni (wanne kushoto), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Sylvester Ambokile (wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na
Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji. Naibu Waziri Masauni alifanya
ziara ya kikazi katika idara hiyo kwa lengo la kujifunza shughuli
mbalimbali zinazofanywa na idara hiyo. Hata hivyo, katika hotuba yake,
aliiagiza idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni
ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la
ajira nchini . Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


0 comments :
Post a Comment