Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine kesho Jumatano
anatarajiwa kuongozana na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na
klabu ya TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta kuelekea nchini Nigeria
kwenye sherehe za utoaji wa tuzo kwa wachezaji
bora barania Afrika.
Mwesigwa anatarajiwa kuondoka na
Samatta kuelekea Nigeria katika mji wa Abuja ambapo sherehe za utoaji
tuzo hizo zitafayika Alhamisi Januari 7, ambapo siku ya sherehe hizo
Katibu Mkuu ataambatana na Ofisa ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria
Mbwana Samatta anawania tuzo ya
mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, huku pia akiwa mfungaji
bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa (CAF CL) baada ya kuifungia klabu
yake ya TP Mazembe mabao 8 na kuibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtakia kila la kheri Mbwana
Samatta katika kinyanganyiro hicho cha uchezaji bora na kusema kwa niaba
ya watanzania wote wanamuombea dua njema aweze kuibuka mchezaji bora wa
Afrika kwa wachezaji wa ndani.
Samatta anawania tuzo ya mchezaji
bora wa Afrika pamoja na mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba
(Congo DR) na mshambuliaji wa Etoile du Sahel Baghdad Boundjah (Algeria)

0 comments :
Post a Comment